Kitengo kinasimamiwa na Mkuu wa Kitengo ambaye anaratibu na kusimamia shughuli zote za TEHAMA.
Eneo la TEHAMA
1.Monitor and maintain active network equipments
Kutathmini mifumo ya mtandao wa kompyuta (Evaluate and troubleshoot network systems).
1.Kutayarisha na kutunza miongozo,taratibu na viwango vya mifumo ya kompyuta.
2.Kusimamia sera, mikakati na miongozo inayotolewa na Serikali Kuu juu ya uendeshaji wa mifumo, miundombinu na vifaa vya TEHAMA;
3.Kuibua mahitaji ya mifumo ili iweze kusanifiwa na kisha kutengenezwa na kutumika;
4.Kuchambua na kuainisha huduma zinazoweza kutolewa na mifumo ya kielekroniki katika Halmashauri;
5.Kuhakikisha mtandao kiambo (Local Area Network) katika Halmashauri inafanya kazi na mtandao wa intaneti unapatikana;
6.Kutengeneza utaratibu mzuri wa kutunza taarifa na data ili ziweze kutumika wakati wa majanga;
7.Kufanya na kusimamia matengenezo ya vifaa vyote vya TEHAMA;
8.Kutoa sifa au viwango vya vifaa kwa ajili ya manunuzi;
9.Kuhakikisha Halmashauri ina tovuti na inapatikana wakati wote.
Eneo la Uhusiano
1.Kusimamia sera, mikakati na miongozo inayotolewa na Serikali Kuu juu ya uendeshaji wa kazi za Uhusiano;
2.Kutangaza kazi na miradi inayofanyika katika Halmashauri;
3.Kutangaza maeneo ya uwekezaji ya Halmashauri katika tovuti, radio na majarida;
4.Kuhakikisha tovuti ya Halmashauri ina taarifa mpya kila wakati.
5.Kuandaa na kutoa majarida kuhusu Halmashauri;
6.Kutumia TEHAMA katika kutoa elimu kwa jamii.
7.Kushauri Halmashauri juu ya uandaaji, uzalishaji na usambazaji wa nyaraka kwa wadau mbalimbali.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.