1 Sekta ya kilimo
Katika Wilaya ya Mvomero eneo linalofaa kwa kilimo ni Hekta 549, 375, eneo linalolimwa kwa sasa ni Hekta 247,219. Kati ya hizo eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji ni Hekta 77,005, aidha eneo linalomwagiliwa kwa sasa ni Hekta 30,802 (hekta 11,188 miundombinu ya kisasa na hekta 19,614 ni mifereji ya asili). Idadi ya Wakulima ni 172,102 ambao kati yao Wanaume ni 82,115 na Wanawake ni 89,987
1.1 Miundombinu ya Umwagiliaji
Wilaya inaendelea na jitihada za kuboresha miundombinu ya umwagiliaji ya kilimo, hususani ya uboreshaji na ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji. Wilaya inazo skimu za umwagiliaji saba zinazoendelezwa katika hatua tofauti. Skimu hizo ni Dakawa, Kigugu, Hembeti/Dihombo, Lukenge, Mkindo, Ndole na Wami Luhindo. Aidha, miundombinu ya skimu ya Mkindo/Mgongola inaendelea kujengwa kwa usimamizi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC). Kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2020/2021 hadi 2022/2023 Wilaya ya Mvomero ilipata jumla ya shilingi 2,698,596,223.50 kutoka kwa Wafadhili mbalimbali wakiwemo Benki ya Dunia, European Union/Helvetas chini ya mradi wa Kuongeza Uzalishaji wa Zao la Mpunga (ERPP) na kupitia mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi Kupitia Mifumo ya Ikolojia Vijijini (EBARR). Fedha hizo zilitumika katika uboreshaji wa miundo mbinu ya umwagiliaji katika skimu ya Kigugu, Hembeti/Dihombo na Lukenge
1.2 Matumizi ya zana bora za kilimo
Wilaya ya Mvomero imeendelea kuwahamasisha Wakulima juu ya matumizi ya zana bora za kilimo, eneo linalolimwa kwa kutumia zana bora za kilimo limeongezeka kutoka asilimia 45 mwaka 2020/2021 hadi asilimia 48 mwaka 2022/2023. Upatikanaji wa zana bora za kilimo umekuwa ukiongezeka kila mwaka.Kwa sasa katika wilaya ya Mvomero kuna jumla ya matrekta makubwa 239, matrekta madogo 87, wanyama kazi 278 na majembe ya wanyama kazi 110.
1.3 Pembejeo za kilimo
Katika msimu wa mwaka 2023/2024 Wilaya ya Mvomero imeendelea kusajili Wakulima katika madaftari kwa ajili ya kupata namba za siri ili kuweza kununua mbolea za ruzuku. Hadi kufikia Desemba 2023 jumla ya wakulima 27,645 walisajiliwa kwenye madaftari na Wakulima 25,049 walikuwa wamesajiliwa kwenye mfumo na kupata namba za kuwawezesha kununua mbolea za ruzuku.
1.4 Hali ya usalama wa chakula wilayani
Mahitaji ya chakula kwa Wakazi 421,741 wa Wilaya ya Mvomero yanakadiriwa kuwa tani 138,542 (tani 100,058 za chakula aina ya wanga na tani 38,484 za chakula aina ya utomwili). Hali ya upatikanaji wa chakula ni ya kuridhisha katika maeneo yote ya Wilaya ambapo vyakula mbalimbali vinapatikana katika hifadhi za binafsi za kaya na sokoni kwa bei rafiki.
1.2 Sekta ya Ushirika
Wilaya ya Mvomero ina jumla vyama vya Ushirika 33 vyenye jumla ya Wanachama 12,753 na vikundi 239. Wanachama hawa na vikundi wana jumla ya hisa zenye thamani ya Tshs. 683,520,000.00 akiba zenye thamani ya Tshs.1,288,208,000.00 na amana zenye thamani ya Tshs. 216,446,000.00
1.2.1 Mikakati ya kukuza Ushirika
1.2.2 Mafanikio katika sekta ya Ushirika
Chama cha Ushirika cha Wakulima wa miwa cha Turiani (TUCOCPRCOS LTD) kimewezeshwa kupatiwa Mkopo wenye thamani ya Tshs.220, 000,000/= ili kununua mashine ya kuvunia miwa (Kameko-Cane loader) kutoka benki ya EFTA na tayari mkopo huo umekwisha rejeshwa.
Kushirikiana kwa ukaribu na vyombo vingine vya Dola kama vile TAKUKURU na Mahakama kuwabana wabadhirifu katika Vyama vya Ushirika na kufanikiwa kurejesha pesa za Chama kiasi cha 123,924,000/= kati ya 461,000,000/= zilizochukuliwa katika Chama cha Akiba na Mikopo cha TURSACCOS kilichopo Turiani. Kiasi kilichobakia kinaendelea kufuatiliwa ili nacho pia kirejeshwe na hatimaye wanachama wafaidike na fedha zao kupitia mikopo.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.