KAZI NA MAJUKUMU YA VITENGO
UTANGULIZI
Idara ya Maendeleo ya Jamii ni miongoni mwa Idara kati ya Idara zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero . Hii ni Idara mtambuka ambapo lengo lake kuu ni kuelimisha wananchi katika mambo mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na kisiasa (kuratibu upatikanaji, usambazaji na utekelezaji wa Sera mbalimbali za Maendeleo). Kuhamasisha jamii kushiriki kwenye shughuli za maendeleo kwa lengo la kujiletea maendeleo yao wenyewe. Idara hii inaamini kwamba maendeleo ya mtu huletwa na mtu mwenyewe, ni imani yetu kwamba watu wanataka mabadiliko na wanaweza kubadilika, lakini hapa ifahamike kwamba mabadiliko yanayolengwa ni mabadiliko ya kimaendeleo na siyo vinginevyo.Idara ya maendeleo ya jamii ina vitengo 6 kama vilivyoainishwa hapa chini, kila kitengo na majukumu yake.
KITENGO CHA UTAFITI, TAKWIMU NA MIPANGO
Kukusanya takwimu mbalimbali za Halimashauri kwa matumizi ya idara
Kufanya uchambuzi wa takwimu
kutoa mafunzo ya uongozi na utawala kwa serikari ya vijiji na mitaa
Kufanya tafiti mbalimbali zenye kuiletea maendeleo jamii
Kuandaa maandiko ya mradi
Uandaaji wa taarifa za robo mwaka na mwaka mzima za idara
Kusimamia kazi, shughuli na utendaji wa kazi wa Maafisa wa Maendeleo ya Jamii walioko kwemye kata
Kumshauri mkuu wa Idara mambo yahusuyo idara ya Maendeleo ya Jamii zikiwemo sera zote za idara na utekelezaji wake.
2. KITENGO CHA MAENDELEO YA WANAWAKE NA WATOTO.
Kusimamia mambo yote yahusuyo maendeleo ya wanawake na watoto katika Halmashauri,
kuratibu sherehe ya siku ya wanawake Duniani,
kuratibu sherehe ya siku ya mtoto wa Afrika,
Kuunda na kuhamasisha uanzishaji wa vikundi vya kiuchumi vya wanawake,
Kusimamia mfuko wa maendeleo ya wanawake kwa utoaji wa mikopo na marejesho yake,
Kutoa taarifa ya maendeleo ya mfuko wa wanawake,
Kusimamia sera za maendeleo ya wanawake na watoto,
Mshauri wa mkuu wa idara juu ya masuala yote yahusuyo maendeleo ya wanawake na watoto.
3. KITENGO CHA MAENDELEO NA JINSIA
Kuelimisha jamii dhana ya jinsia na kuratibu sherehe ya siku ya familia,
Kuelimisha jamii juu ya dhana potofu ya mila na desturi zinazoathiri jamii kimaendeleo,
Kutoa elimu/mafunzo na uhamasishaji wa dhana ya lishe kwa jamii kwaajili ya kuleta maendeleo katika jamii,
Mshauri wa mkuu wa idara juu ya sera na utekelezaji wake kwa masuala yote yahusuyo jinsia,
4. KITENGO CHA USTAWI WA JAMII
Kusimamia utambuzi wa watoto walioko katika mazingira hatarishi kwa kuwa na takwimu za mara ( yatima, watoto wa mtaani),
Kufanya utambuzi wa makundi maalumu kama wazee,wajane,wagane,wenye ulemavu
kuratibu sherehe ya siku ya wazee Duniani
Kutoa huduma (service delivery) kwa jamii/familia zenye migogoro ya ukosefu wa huduma za watoto
Kuielimisha jamii juu ya sheria ya mtoto, ajira za watoto
Kusimamia utaratibu wa PAROLI- wafungwa wanaostahili kuwa nje ya magereza kwa kufanya kazi za kiserikali wakiwa kifungoni
Kuwa na mipango endelevu ya kupunguza kasi ya ongezeko la watoto wa mitaani
Kusimamia shughuli za ustawi wa jamii kwa wananchi/jamii
Kumshauri mkuu wa idara masuala yote yahusuyo ustawi wa jamii
5. KITENGO CHA UJENZI VIJIJINI
Kufanya utambuzi wa mafundi vijijini kwa fani zao(uashi,ufundi seremala ) pamoja na viwanda vidogo vidogo
Kutoa mafunzo ya mafundi juu ya ujenzi wa nyumba bora zenye gharama nafuu
Kuelimisha serikali za vijiji juu ya ujenzi wa makazi bora ya nyumba bora vijijini
Kusimamia upatikanaji wa ramani na usambazaji wa ramani za nyumba bora vijijini kwa serikali za vijiji
Kuunda vikosi vya ujenzi kwenye kata (building brigades) ili wasimamie kazi za ujenzi wa majengo ya serikali
Usambazaji wa teknologia sahihi kwa wananchi vijijini(majiko bora na banifu, zana bora za kazi)
Kumshauri mkuu wa idara masuala yote yahusuyo ufundi na ujenzi vijiji
6. KITENGO CHA VIJANA
Kuhamasisha juu ya sera ya vijana
Kushirikiana na Afisa utamaduni juu ya masuala ya maedndeleo ya vijana
Kuhamasisha uundaji wa vikundi vya vijana
kusimamia utoaji mikopo kwa vijana na marejesho yake
Kufanya utambuzi wa vikundi vya vijana na shughuli zao za kiuchumi
Kutoa elimu/ mafunzo ya ujasriamali kwa vikundi vya vijana
Kumshauri mkuu wa idara masuala yote yahusuyo maendeleo ya vijana
MIRADI INAYOTEKELEZWA NA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII NA MAJUKUMU YA WARATIBU WA MIRADI
KITENGO CHA UKIMWI
Kuhamasisha na kuelimisha jamii juu ya kupunguza kasi ya maambukizi mapya ya UKIMWI
kuratibu mafunzo kwa kamati za kudhibiti UKIMWI za VMAC/WMAC/CMAC
Kutekeleza kazi zote za UKIMWI kama zilivyo kwenye sera ya UKIMWI
Kumshauri mkuu wa idara kuhusu masuala ya UKIMWI
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.