Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mvomero Bi. Mary Kayowa leo Agosti 19, 2025 amekabidhi fomu ya uteuzi kwa Mgombea wa Kiti cha Ubunge kupitia Chama Cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo) Bw. Kashikashi Saimanga Ligowoka. Zoezi hilo imefanyika katika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mvomero.
Aidha, Mgombea huyo ameambatana na Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Mvomero Bw. Edgar Rogath Malubuta.
Sambamba na zoezi hilo, usajili wa wagombea katika mfumo wa usimamizi wa wagombea yaani CMS, limeendelea kwa ushirikiano wa Maafisa TEHAMA, Afisa Uchaguzi na Msimamizi wa Uchaguzi.
"Kura yako Haki yako, Jitokeze kupiga kura"
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.