Zoezi la utoaji wa fomu za uteuzi kwa wagombea Ubunge na Udiwani Jimbo la Mvomero linaendelea kushika kasi ambapo leo Agosti 20, 2025, Mgombea Ubunge kupitia chama cha Makini Bw. Godfrey Joseph Juma amekabidhiwa fomu za uteuzi na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mvomero Bi. Mary Kayowa. Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi.
Sambamba na zoezi hilo, usajili wa Wagombea kwenye mfumo wa Usimamizi wa Wagombea yaani CMS linaendelea kwa ushirikiano wa Maafisa TEHAMA, Afisa Uchaguzi pamoja na Msimamizi wa Uchaguzi.
Zoezi hilo la utoaji wa fomu za uteuzi litahitimishwa Agosti 27, 2025."Kura yako Haki yako, Jitokeze kupiga kura"
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.