Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mhe. Maulid Dotto, ameahidi kushirikiana na wadau mbalimbali kutafuta eneo maalum litakalotumika kwa ajili ya mashindano ya mbio za magari wilayani humo.
Akizungumza Agosti 17, 2025 wakati akifunga rasmi mashindano hayo ambayo yaliaanza Agosti 16, 2025 Mhe. Dotto amesema Serikali inatambua mchango wa michezo ya magari katika kujenga vipaji, kutoa burudani na kuchochea uchumi kupitia uwekezaji na utalii wa ndani.
Aidha, kwa kutambua mchango huo amewataka waandaaji wa michezo hiyo kuwasilisha barua katika ofisi yake ikiahinisha sifa za eneo linalofaa kwa ajili ya michezo ya magari.
“...niwaombe wahusika kuleta suala hilo kwangu kwa kuniandikia barua ambayo itaahinisha sifa na ukubwa wa eneo linalohitajika ili nami niweze kupata nafasi ya kuangalia kama katika wilaya ya Mvomero tunaweza kupata eneo la kumiliki ninyi wenyewe..." amesema Mkuu waWilaya.
Sambamba na hilo amewapongeza viongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Walaya ya Mvomero kupitia shamba la miti Morogoro kwa kutoa eneo lao kwa ajili ya mashindano hayo kwani yanahamasisha utalii wa ndani.
Kwa upande wao, wadhamini wa mashindano hayo wamesema lengo la mashindano hayo ni kuwaleta pamoja wadau mbalimbali pamoja na kutoa fursa kwa watu wakiwemo wajasiliamali hususan wakati wa mashindano. Wameongeza kuwa changamoto kubwa ni kukosa eneo maalum la kufanyia mashindano hayo jambo linalosababisha kutofikia malengo.
MWISHO
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.