1 Sekta ya Mifugo
Wilaya ya Mvomero inakadiriwa kuwa na jumla ya Wafugaji 18,749 ambao wanamiliki jumla ya Ng’ombe 201,410, Mbuzi 84,180, Kondoo 13,627 na Punda 2,128. Eneo la Wilaya ni Ha. 732,500 na eneo linalofaa kwa ufugaji ni Ha. 266,400 lenye uwezo wa kulisha ng’ombe 133,200 kwa mwaka. Eneo hili ni pungufu kwa Ha. 136,420 kulingana na idadi ya Ng’ombe waliopo kwa sasa, ambapo ng’ombe 1 anahitaji hekta 2 za malisho kwa mwaka.
1.2 Uzalishaji wa nyama na maziwa.
Wilaya ina machinjio ndogo 7 na machinjio kubwa 1 inayomilikiwa na kampuni ya (Nguru Hills Ranch). Kwa wastani idadi ya wanyama wanaochinjwa kwa mwaka ni 40,765 katika machinjio ndogo.
Wilaya ya Mvomero ina jumla ya ng'ombe wa maziwa 10,744. Wastani wa uzalishaji wa maziwa ndani ya Wilaya kwa mwaka ni maziwa ya ng’ombe lita 10, 697,400 na maziwa ya mbuzi lita 135,040.
1.3 Miundombinu ya Mifugo
Katika kuboresha utoaji huduma kwa Wafugaji na mifugo yao, Wilaya kwa kushirikiana na wadau imejenga na kuimarisha miundombinu mbalimbali ya mifugo.Kwa sasa wilaya ya Mvomero inayo jumla ya majosho 24, makaro ya kuchinjia 10, machinjio ndogo 7, vituo vya kukusanyia maziwa 12 , malambo ya kunyweshea mifugo 16 na minada ya mifugo 5 .
1.4 Dawa za ruzuku za kuogesha mifugo.
Kwa kipindi cha mwaka 2021 hadi 2022 Wilaya imepokea toka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi dawa za ruzuku za kuogesha mifugo lita 120. Matumizi ya dawa hizi yamepunguza vifo vya mifugo vinavyotokana na magonjwa ya kupe kwa asilimia 50.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.