Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amezitaka Halmashauri zote mkoani humo kuhakikisha mipango na bajeti wanazoandaa zinaendana na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 ili kuchochea maendeleo endelevu na jumuishi kwa wananchi.

Mhe. Malima ametoa agizo hilo Januari 27, 2026 wakati wa kikao cha tathmini ya utendaji kazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halimashauri.
Mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza kuwa ufanisi wa maendeleo ya wananchi unatokana na mipango bora inayotekelezwa kwa kuzingatia vipaumbele vya Wilaya, Mkoa na taifa. Huku akibainisha kuwa mipango isiyolingana na dira ya taifa inaweza kusababisha matumizi yasiyo na tija ya rasilimali za umma.

“…tuntaka hiyo mliyotuletea na takwimu mlizoandika ziendane na Dira ya Taifa 2050…” amesema Mkuu wa Mkoa.
Naye Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Usimamizi, ufuatiliaji Bi. Neema Dachi ameainisha vigezo vinavyotumika kupima utendaji kazi wa Halmashauri mbalimbali ikiweo ukusanyaji wa mapato, utengaji wa fedha za miradi ya maendeleo, miradi iliyotekelezwa kuanzia mwaka wa fedha wa 2021/2022 hadi kufikia 2025/2026 mwezi Disemba 2025, utekelezaji wa miradi viporo ya Serikali kuu na mapato ya ndani.
Aidha, ameongeza kuwa vipaumbele vingine ni pamoja na utoaji wa mikopo ya asilimia 10 na marejesho yake, utoaji wa fedha za lishe, utoaji wa taulo za kike, utoaji wa vyandarua na utoaji wa vyakula mashuleni, utekelezaji wa miradi ya Mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) pamoja na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Ndg. Paulo Faty ameahidi kuyafanyia kazi maelekezo na maagizo yaliyotolewa na Viongozi wa Mkoa ili kuhakikisha kuwa Halmashauri hiyo inafikia malengo yake ya kutoa huduma bora kwa wananchi.
MWISHO
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.