• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
MVOMERO DISTRICT COUNCIL
MVOMERO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Afya
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Uongozi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Teknolojia,Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
    • Baraza la Madiwani
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Rasilimali Watu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Itakayo tekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Viwanda
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti

DC MVOMERO ALIPONGEZA SHIRIKA LA SAWA KUJENGA MADARASA YA SHULE SHIKIZI, AAGIZA MCHAKATO WA USAJILI UANZE MARA MOJA

Posted on: January 23rd, 2026

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mhe. Maulid Dotto, amelipongeza Shirika la SAWA WANAWAKE TANZANIA kwa jitihada zake za kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu wilayani humo kupitia ujenzi wa madarasa ya shule shikizi katika eneo la Kwa Wagogo hatua hiyo itasaidia kupunguza changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kupata elimu

Mhe. Maulid Dotto ametoa pongezi hizo Januari 23, 2026 wakati wa hafla ya kupokea mradi huo uliojengwa kwa ushirikiano wa Shirika la SAWA pamoja na wananchi wa eneo hilo.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema ujenzi wa miundombinu hiyo ni mfano wa ushirikiano mzuri kati ya Serikali na wadau wa maendeleo, akisisitiza kuwa shirika hilo limekuwa la kizalendo kwa kutatua changamoto za watoto wa kitanzania ambao wamekuwa wakipata adha ya kupata elimu.

Aidha, amemuagiza mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kuhakikisha mchakato wa usajili wa shule hiyo unaanza mara moja ili kuwezesha watoto kuanza masomo kwa wakati, sambamba na kukamilisha taratibu zote za kisheria na kiutawala.

Sambamba na hilo, Mkuu wa Wilaya amewahimiza wananchi wa eneo hilo kuendelea kujitoa kuchangia ujenzi wa madarasa mengine ili shule hiyo iweze kujitegemea kama shule nyingine na kutunza miundombinu hiyo ili iweze kudumu. Pia, amesitiza kuwa Serikali ya Wilaya itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu kwa Shirika la SAWA na wadau wengine ili kuhakikisha miradi ya elimu inatekelezwa kwa ubora na kwa kuzingatia malengo ya Serikali ya kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa watoto wote.

Naye, Mkurugenzi wa Shirika hilo, Bi. Helen Mkalang'ambo ameushukuru uongozi wa Wilaya ya Mvomero kwa ushirikiano wanaoupata wakati wa kutekeleza miradi yao, huku akibainisha kuwa mradi huo umehusisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, ofisi pamoja na matundu vya vyoo, aidha, shirika limekamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ambavyo vimejengwa kwa nguvu ya wananchi.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Dakawa Mhe. Joshua Lugaso amemshukuru Mkurugenzi wa shirika hilo pamoja na wananchi wa eneo hilo la Kwa wagogo kwa ushirikiano wao hadi kufanikisha

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 14, 2025
  • MAJINA YA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WALIOITWA KWENYE USAILI OKTOBA 17, 2025 October 14, 2025
  • MAJINA YA RESERVE WA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WANAOTAKIWA KWENYE USAILI KATIKA KATA October 14, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MIPANGO, BAJETI ZA HALMASHAURI ZIENDANE NA DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050 - RC MALIMA

    January 27, 2026
  • DC MVOMERO ALIPONGEZA SHIRIKA LA SAWA KUJENGA MADARASA YA SHULE SHIKIZI, AAGIZA MCHAKATO WA USAJILI UANZE MARA MOJA

    January 23, 2026
  • KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO YAKAGUA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO SEKTA ZA AFYA, ELIMU

    January 22, 2026
  • WAZAZI/WALEZI WAELIMISHWE JUU YA UMUHIM WA CHAKULA SHULENI ILI WAHAMASIKE KUCHANGIA

    January 19, 2026
  • Tazama Zote

Video

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kimkoa yafanyika Halimashauri ya Wilaya Mvomero
Video Zaidi

Viungo vya Haraka

  • Ukurasa wa Facebook

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais Ikulu
  • Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira
  • Baraza la Mtihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero

    Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO

    Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348

    Mobile: +255 23 293 4348

    Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani Eneo
    • Huduma

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.