Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mhe. Koira Kurman Majuka ameongoza kikao cha Baraza la Kata kujadili taarifa za Kata kwa robo ya Pili kipindi cha Oktoba - Desemba kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Kikao hicho kimefanyika leo Januari 29, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri kikiwakutanisha Waheshimiwa Madiwani, Watendaji wa Kata 30 za Halmashauri hiyo, pamoja na Wataalam wa Halmashauri.



Akizungumza wakati akifungua kikao hicho Mhe. Koila amewataka watendaji wa Kata na Wataalam wa Halmashauri kuteleleza majukumu yao kwa weledi na kuhakikisha kuwa hakuna migongano baina ya watendaji kwa watendaji ama watendaji na Madiwani ili halmashauri hiyo iweze kuwaletea maendeleo wananchi wa Wilaya hiyo.

Kata zilizowasilisha taarifa zake ni pamoja na Kata ya Mtibwa, Kanga, Sungaji, Mvomero, Mkindo, Dakawa, Kikeo, Tchenzema, Nyandira, Mzumbe na Mlali huku Kata nyingine zitawasilisha taarifa zake katika kikao kijacho.








Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.