1 Huduma za Afya Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati)
Idara ya Afya inatoa huduma za afya ya tiba na kinga. Upande wa afya kinga kuna huduma za afya ya uzazi na mtoto,usafi wa mazingira, UKIMWI,kifua kikuu na ukoma,Malaria na huduma za afya shuleni.Wilaya ya Mvomero ina jumla vituo vya kutolea huduma za afy 83.ikiwa na hospitali 3 vituo vya afya 10 na zahanati 70
Jedwali Na.16: Idadi ya hospitali, vituo vya afya na zahanati
JINA LA KITUO
|
SERIKALI
|
MASHIRIKA YA DINI
|
BINAFSI
|
JUMLA
|
Hospitali
|
1
|
1
|
1
|
3
|
Vituo vya afya
|
8
|
2
|
0
|
10
|
Zahanati
|
57
|
7
|
6
|
70
|
JUMLA
|
66
|
10
|
7
|
83
|
7.2 Hali ya Watumishi
Sekta ya afya ina mahitaji ya watumishi 1052 wa kada mbalimbali, mpaka sasa kuna watumishi 519 na hivyo kufanya upungufu wa watumishi 533
7.3 Miradi ya maendeleo (miundombinu) iliyotekelezwa katika kipindi cha kuanzia Julai 2021 hadi Desemba 2023
Katika kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha Julai 2021 hadi Desemba 2023 Wilaya ya Mvomero imefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu katika sekta ya afya. Jumla ya kiasi cha Tsh 3,073,000,000.00 zimetolewa kwenye ujenzi wa miundombinu ya afya na jumla ya majengo 28 yamejengwa kama inavyoonekana kwenye jedwali Na.17 hapa chini.
Jedwali Na 17: Miradi ya Maendeleo (Miundombinu) iliyotekelezwa katika Sekta ya Afya
Jina la mradi
|
Aina ya majengo yaliyojengwa
|
Idadi ya majengo yaliyojengwa
|
Kiasi cha fedha kilichotolewa
|
Ujenzi wa hospitali ya Wilaya
|
|
7
|
1,440,000,000
|
Ujenzi wa kituo cha afya Mziha
|
|
6
|
500,000,000
|
Ujenzi wa kituo cha afya Dakawa
|
1.Jengo la wagonjwa wa nje
2.Jengo la maabara 3.Kichomea taka |
3
|
275,000,000
|
Uboreshaji wa kituo cha afya Mlali
|
1.Jengo la upasuaji
2. Jengo la wazazi 3.Jengo la maabara 4.Nyumba ya watumishi 5.Jengo la kuhifadhia maiti 6.Kichomea taka |
6
|
558,000,000
|
Ukamilishaji ujenzi wa zahanati 6 za Kidudwe,Manyinga, Misengele,Difinga,Tchenzema na Ndole
|
Zahanati
|
6
|
300,000,000
|
JUMLA
|
|
|
3,073,000,000
|
7.4 Mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa (ICHF)
Mfuko wa Afya ya Jamii CHF iliyoboreshwa ilizinduliwa tarehe 1/7/2019 katika halmashauri ya wilaya ya Mvomero , kama ilivyo katika Mwongozo kila kaya yenye watu 6 hujiunga kwa Tshs 30,000/= kwa ajili ya kupata huduma za afya kwa mwaka mzima.Hadi kufikia Desemba 2023 ,jumla ya kaya 16,410 zimejiunga na mfuko wa CHF kati ya kaya 72,519 zilizopo Wilayani Mvomero. Idadi hii ya kaya ni sawa na asilimia 23 ya kaya zote zinazotakiwa kujiunga na mfuko wa Ichf. Aidha kiasi cha fedha iliyokusanya katika huu mfuko katika hiki kipindi ni Tshs 93,390,000.00
7.5 Mfumo wa Serikali wa taarifa za wagonjwa na ukusanyaji wa mapato (Got-homis)
Hadi kufikia Oktoba 2023 mfumo wa Got-homis umefungwa katika vituo vya kutolea huduma za afya 13 na unafanya kazi. Vituo hivyo ni Hospitali ya wilaya,Kituo cha afya Mvomero,Kituo cha afya Kibati, Kituo cha afya Mgeta, Kituo cha afya Mlali,Kituo cha afya Melela, zahanati ya Lusanga, zahanati ya Milama, zahanati ya Nyandira,zahanati ya Mkindo
7.6 Msamaha ya wagonjwa.
Makundi ya Wagonjwa wa Msamaha ni kina mama wajawazito,watoto chini ya miaka 5, magonjwa sugu, wazee na walemavu. Katika kipindi cha kuanzia Julai 2021 hadi kufikia Desemba 2023, thamani ya fedha zilizotolewa msamaha kwa makundi haya ya wagonjwa ni kiasi cha Tsh 289,368,000.00
7.7 Hali ya upatikanaji wa dawa
Hali ya upatikanaji wa dawa ni ya kuridhisha, mpaka kufikia Desemba 2023 upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ilikuwa ni 92% na upatikanaji wa dawa za msingi ilikuwa 95 % .
Huduma ya baba, mama na mtoto inatolewa katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma za Afya Wilayani. Huduma zinazotolewa ni pamoja na:-
7.8.1 Mafanikio ya utoaji huduma ya afya ya uzazi na mtoto wilayani kwa kipindi cha Julai 2021 hadi Desemba 2023
7.9 Magonjwa ya mlipuko
Katika kipindi cha kuanzia Julai 2021 Oktoba 2023 jumla ya wagonjwa 53 walihisiwa kuwa na ugonjwa wa surua katika vijiji vya Mkindo na Wami Dakawa.Ufuatiliaji ulifanyika na hatua za kuzuaia maambuzi kuendelea kuenea zilichukuliwa
7.9.1 Mikakati ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko
Katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko Halmashauri inaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujikinga na kuzuia milipuko kwa kuzingatia kanuni za afya kupitia mbinu shirikishi (Community led total sanitation). Aidha, kuna utoaji wa chanjo mbalimbali kwa watoto na akina mama kwenye vituo vya kutolea huduma, kuzuia magonjwa ya mlipuko mfano surua
7.10 Hali ya maambukizi ya VVU na UKIMWI Wilayani Mvomero
Kiwango cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi Wilayani bado ni kikubwa. Wilaya kwa kushirikiana na wadau wake wa maendeleo inaendelea kuelimisha jamii jinsi ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ukimwi hasa vijana na kutoa huduma kwa walioathirika na VVU. Wilaya ya Mvomero inavyo vituo 83 vya utoaji wa dawa dhidi ya virusi geuzi (hospiali 3 vituo vya afya 10 na zahanati 70
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.