Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mvomero Bi. Mary Kayowa leo Agosti 26, 2025 amekabidhi fomu za uteuzi kwa mgombea Ubunge kupitia chama cha Mapinduzi - CCM Bi. Sarah Msafiri Ally. Zoezi hilo limefanyika katika ofisi ya msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mvomero.
Aidha, Mgombea huyo ameambatana na Katibu wa Chama hicho Ndg. Florance Machicho pamoja na baadhi ya wajumbe Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Mvomero.
Sambamba na hilo, zoezi la usajili wa wagombea katika mfumo wa usimamizi wa wagombea (CMS) limeendelea kwa ushirikiano wa Maafisa TEHAMA, Afisa Uchaguzi na Msimamizi wa Uchaguzi.
Kwa mujibu wa ratiba ya iliyotolewa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi - INEC zoezi la utoaji wa fomu za uteuzi kwa wagombea wa nafasi ya Ubunge na udiwani litahitimishwa tarehe 27 Agosti, 2025.
"Kura yako Haki yako, Jitokeze kupiga kura"
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.