• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
MVOMERO DISTRICT COUNCIL
MVOMERO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Afya
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Uongozi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Teknolojia,Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
    • Baraza la Madiwani
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Rasilimali Watu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Itakayo tekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Viwanda
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti

Huduma za Elimu

SEKTA YA ELIMU

1  Elimu ya  awali na Msingi

 1.1 Idadi ya shule za Msingi 2021-2023

Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero  ina shule za msingi 164 Kati ya shule hizo shule 154 ni za Serikali na 10 ni za watu au mashirika binafsi/dini 

1.2  Idadi ya Wanafunzi wa Shule za Msingi 2021 – 2023

Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kwa   mwaka 2023 ina jumla ya wanafunzi 93022 wa shule za msingi wavulana wakiwa 45,645 na wasichana 47377 kukiwa na  ongezeko la wanafunzii 3670  ikilinganishwa na mwaka 2021

1.3   Uandikishaji wa Darasa la I mwaka  2023 na 2024

Halmashauri ya wilaya ya Mvomero  kwa mwaka 2023 ilikuwa na lengo la kuandikisha wanafunzi darasa la kwanza 12757 Kati yao wavulana wakiwa 6439 na wasichana 6318 Wanafunzi walioandikishwa na kuanza darasa la I ni  12966 wavulana wakiwa  wavulana 6404 na wasichana  6462 idadi hii ni sawa na asilimia 101 ya lengo la mwaka.  Katika mwaka 2024 Halmashauri imeweka lengo la kuandikisha wanafunzi. 11,871 kati yao wavulana wakiwa  6007 na wasichana 5864  Hadi kufikia Januari 6, 2024 jumla ya wanafunzi 10,352 wameandikishwa, wavulana wakiwa 5466 na wasichana wakiwa 4886

1.4  Majengo ya Shule za Msingi na Samani  hadi  Desemba 2023

Wilaya ya Mvomero  inaendelea kuongeza vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo, nyumba za walimu na samani hususani madawati ya wanafunzi ili kuboresha mazingira ya kutolea elimu. Kwa sasa kuna jumla ya vyumba vya madarasa  1006 matundu ya vyoo 1416  nyumba za walimu 370 na madawati 25200.

Jedwali Na 1: Hali ya majengo katika shule za msingi mwaka 2023

Aina ya Jengo
Mahitaji
Vyumba vilivyopo
Upungufu
 Asilimia za upungufu       %
Vyumba vya madarasa
2067
1006
1064
51.5
Nyumba za walimu
2067
370
1697
32
Matundu ya vyoo
4374
1416
2958
68
Matundu ya vyoo vya walimu
308
196
112
36

 

Jedwali Na.2 : Hali ya madawati mwaka 2021-2023

Mwaka
Idadi ya Wanafunzi
Mahitaji ya Madawati
Madawati Yaliyopo
Upungufu wa Madawati
2021
89352
29784
20009
4584
2022
92164
30721
22400
8321
2023
93022
31007
25200
4584

 

  1.5 Hali ya Taaluma katika Shule za Msingi mwaka 2020 - 2023

 Hali ya taaluma katika shule za msingi  imekuwa ikiimarika kila mwaka. Kwa kipindi cha miaka 3 kuanzia mwaka 2021 hadi 2023 katika wilaya ya Mvomero hali ya ufaulu kwa wanafunzi wanaomaliza Elimu ya Msingi imekuwa ikipanda Jedwali Na. 3 linaonesha hali halisi ya kufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi wilayani:

Jedwali Na 3.  Ufaulu wa wanafunzi kutoka mwaka 2021 hadi 2023

Mwaka
Waliofanya Mtihani
              Waliofaulu
Waliochaguliwa Kuingia     Kidato Cha I
Wav
Was
Jml
Wav
Was
Jml
%
Wav
Was
Jml
%
2021
3971
4333
8304
2858
3136
5994
72.19
2858
3136
5994
100
2022
4809
5180
9989
3219
3567
6786
68
3219
3567
6786
100
2023
5061
5556
10617
3383
3833
7216
68
3383
3833
7216
100

1.6 Idadi   ya walimu wa shule za msingi kwa mwaka 2023

Halmashauri ya wilaya ya Mvomero ina uhitaji wa walimu 2067 kwa shule za msingi na awali. Walimu waliopo sasa ni 1511 hivyo kuna upungufu wa walimu 556 Jedwali  Na 4 hapa chini linaonyesha idadi ya walimu.

  • Jedwali Na 4: Hali ya walimu shule za msingi
Mwaka
Mahitaji
Waliopo
Asilimia
Upungufu
2021
1986
1366
67
620
2022
2048
1535
75
513
2023
2067
1511
73
556
  •  1.7 Elimu Bila Malipo

Kwa kipindi cha kutoka Julai 2021 hadi Desemba 2023 Wilaya ya Mvomero imepokea jumla ya Tsh  2,410,431,332.16 za elimu bila malipo kwa ajili ya uendeshaji wa Shule za Msingi katika maeneo ya Ruzuku ya uendeshaji, ruzuku  ya chakula na Posho ya madaraka ya walimu wakuu na maafisa elimu kata .

  • Jedwali Na.5:   Mapokezi ya fedha za Elimu bila malipo kuanzia Julai 2021 hadi Desemba  2023 
 MWAKA
FEDHA ZA ELIMU BILA MALIPO ZILIPOKELEWA   
2021/2022
1,033,901,418.34
2022/2023
1,055,745,328.82
2023/2024 KUISHIA OKTOBA 2023
320,784,585
JUMLA
2,410,431,332.16
  •  
  • 1.8 Miradi ya maendeleo (miundombinu) iliyotekelezwa katika kipindi cha kuanzia Julai 2021 hadi Desemba  2023
  • Katika kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha Julai 2021 hadi Desemba 2023 Wilaya ya Mvomero imepokea jumla ya Tsh 2,812,684,464 kwa ajili ya  kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu katika Divisheni ya elimu awali na msingi kama inavyoonekana kwenye Jedwali  Na 6 hapa chini.
  •  
  •  
  •  

Jedwali Na.6: Miradi ya Maendeleo (Miundombinu) iliyotekelezwa katika Divisheni ya elimu awali  na msingi

Jina la mradi
Aina ya majengo yaliyojengwa
Idadi ya majengo yaliyojengwa
Kiasi cha fedha kilichotolewa
Ujenzi  wa vyumba vya madarasa 99 katika shule za msingi
Vyumba vya madarasa
74
1,498,974,000
Ujenzi wa shule mpya 2 za msingi
Vyumba vya madarasa 25, majengo ya utawala 2, vyoo matundu  40
33
782,200,000
Ujenzi wa nyumba za walimu
Nyumba za walimu (2 in 1)
6
300,000,000
Ujenzi wa bweni 1 la wanafunzi wenye mahitaji maalum shule ya msingi changarawe
bweni
1
98,480,834

 

2 ELIMU YA SEKONDARI

 2.1 Idadi ya shule za Sekondari, Walimu na wanafunzi mwaka 2023

Wilaya ya  Mvomero  ina jumla ya shule za sekondari 34 kati ya shule hizo shule 31 ni za Serikali na shule 3 ni watu/taasisi binafsi na mashirika ya dini. Kwa mwaka 2023 wilaya ya Mvomero ina jumla ya wanafunzi wa sekondari 18,223 (ke 9,622 na me 8,601)kati yao wanafunzi  17,729 (ke 9,371na me 8,358) wanasoma katika shule za sekondari za serikali na wanafunzi  494 (ke 251 na ke 243) wanasoma katika shule za sekondari za watu/taasisi binafsi na mashirika ya dini. Aidha kwa sasa Wilaya ya Mvomero ina jumla ya walimu wa shule za sekondari  784 (ke 291 na me 493) kati yao walimu  746 (ke  271 na me 475) wanafundisha katika shule za sekondari za serikali na walimu 38 (ke 20na me 18 ) wanafundisha katika shule za sekondari za watu/taasisi binafsi na mashirika ya dini.

2.2 Wanafunzi waliojiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023

Wanafunzi waliojiunga kidato cha kwanza kwa mwaka 2023  ni  5950 sawa na asilimia  85 ya wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza  mwaka 2023 ambao walikuwa wanafunzi 7005

2.3 Madarasa, Nyumba za walimu , Vyoo  na viti na meza  katika Shule za Sekondari  hadi Mwezi  Desemba 2023

 

Wilaya imeendelea kuongeza kila mwaka vyumba vya madarasa, nyumba za walimu na matundu ya vyoo katika shule za sekondari. Hadi kufikia Desemba 2023 palikuwa na jumla ya vyumba vya madarasa 527 nyumba za walimu 81 matundu ya vyoo  751 meza 18,875 viti 18,278

 

 

Jedwali Na. 7:  Hali ya vyumba vya madarasa, nyumba za walimu na vyoo hadi  Desemba 2023

Mwaka
Madarasa
Nyumba za walimu
Matundu ya vyoo
Mahitaji
yaliyopo
Upungufu
Mahitaji
zilizoopo
Upungufu
Mahitaji
Vilivyopo
Upungufu
2023
556
527
29
746
81
665
902
751
151

 

Jedwali Na. 8: Hali ya Samani hadi kufikia Desemba 2023

Mwaka
Meza
                         Viti
Mahitaji
Yaliyopo
Upungufu
Mahitaji
Yaliyopo
Upungufu
2023
17,729
18,875
0
17,729
18,278
0

 

 2.4 Majengo ya maabara, maktaba na Utawala mwaka 2023

Wilaya inaendelea kuongeza majengo ya maabara ,Maktaba na majengo ya utawala. Hadi kufikia Oktoba 2023 Wilaya ina jumla ya majengo ya utawala 7 yaliyokamilika na yanatumika na mengine 2 ambayo katika hatua mbalimbali za ujenzi, maktaba 1 iliyokamilika na inafanya kazi na 2 .zilizo katika hatua mbalimbali za ujenzi na pia ina maabara 51 zilizokamilika na zinatumika na maabara 6 zilizo katika hatua mbalimbali za ujenzi

Jedwali Na.9: Hali ya Majengo ya Maabara na utawala mwaka Desemba  2023

Mwaka
Maabara
Maktaba
 
Majengo ya utawala
Mahitaji
Zilizopo
Mahitaji
Yaliyopo
Mahitaji
Yaliyopo
2023
93
51
31
1
31
7








 

 2.5 Ufaulu wa wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne na sita kutoka mwaka 2020 hadi 2023

Kuanzia mwaka  2020 hadi 2023  ufaulu wa wanafunzi umekuwa ukipanda kama inavyoonesha katika jedwali Na 11  na Na 11  hapo chini.

Jedwali.Na.10: Ufaulu wa wanafunzi kidato cha nne mwaka 2020 hadi  2023

Mwaka
Idadi ya shule zenye kidato cha IV
Idadi ya wanafunzi waliofanya Mtihani
Wanafunzi wal1869iofaulu
Wanafunzi wasiofaulu
% ya Ufaulu
2020
25
2367
1869
451
78.96
2021
25
2542
2081
461
81.8
2022
26
4071
3139
932
77

 

 

 

Jedwali.Na.11: Ufaulu wa wanafunzi kidato cha sita mwaka 2020 hadi  2023

Mwaka
Idadi ya shule zenye kidato cha VI
Idadi ya wanafunzi waliofanya Mtihani
Wanafunzi waliofaulu
Wanafunzi wasiofaulu
% ya Ufaulu
2020
2
184
184
0
100
2021
3
280
279
1
99.9
2022
3
340
340
0
100
2023
4
439
439
0
100

 

   2.6 Elimu Bila Malipo

Kwa kipindi cha kutoka Julai 2021 hadi Desemba 2023 Wilaya ya Mvomero imepokea jumla ya Tsh 2,736,223,594.40 za elimu bila malipo kwa ajili ya uendeshaji wa Shule za Sekondari  katika maeneo ya Ruzuku ya uendeshaji, ruzuku  ya chakula, Posho ya madaraka ya wakuu wa shule, fidia ya ada pamoja na ruzuku ya mitihani.

 

 

Jedwali Na. 12: Mapokezi ya fedha za Elimu bila malipo kuanzia Julai 2021 hadi Desemba 2023 

 MWAKA
FEDHA ZA ELIMU BILA MALIPO ZILIPOKELEWA  
2021/2022
1,056,304,601.30
2022/2023
1,280,067,309.20
2023/2024 KUISHIA  DESEMBA 2023
399,851,594.40
JUMLA
2,736,223,594.40

 

 

2.7 MIRADI YA MAENDELEO (MIUNDOMBINU) ILIYOTEKELEZWA KATIKA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI 2021 HADI DESEMBA 2023

Katika kipindi cha kuanzia Julai 2021  hadi  Desemba 2023 Wilaya ya Mvomero imepokea fedha kiasi cha Tsh 5,777,295,495 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu katika divisheni  ya Elimu Sekondari  kama inavyoonekana kwenye jedwali Na. 13  hapa chini.

Jedwali Na 13:  Miradi ya Maendeleo (Miundombinu) iliyotekelezwa katika sekta  ya Elimu Sekondari

JINA LA MRADI
AINA YA MAJENGO YALIYOJENGWA
IDADI YA MAJENGO YALIYOJENGWA
KIASI CHA FEDHA KILICHOTOLEWA
Ujenzi na ukamilishaji wa miundombinu shule ya sekondari ya Sokoine memorial
Maabara 3,uzio,bwalo 1 na bweni 1
6
600,000,000
Ujenzi wa mabweni katika shule za sekondari za Lusanga,Doma na Pemba
Mabweni
3
370,000,000
Ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule  za sekondari 26
Madarasa
174
3,480,000,000
Ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Homboza
Madarasa 8, maabara 3, jengo la utawala,jengo la maktaba, jengo la ICT, vyoo matundu 20, nyumba ya mwalimu
18
565,000,000
Ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Kweuma
Madarasa 8, maabara 3, jengo la utawala,jengo la maktaba, jengo la ICT, vyoo matundu 20
17
528,998,425
Ukamilishaji wa maabara 15  katika shule 5 za sekondari
Maabara
15
150,000,000
Ujenzi wa vyoo matundu 59 katika shule 10 za sekondari
Matundu ya vyoo
59
83,300,000
JUMLA
 
 
5,777,298,425

 

Matangazo

  • MAJINA YA WAANDISHI WASAIDIZI NA BVR KIT OPERATORS. February 22, 2025
  • Majina ya Waandishi wasaidizi na BVR KIT Operators February 22, 2025
  • Kuitwa Kwenye Usahili Nafasi Ya Mtendaji Wa Kijiji,Mtunza Kumbukumbu,Afisa Hesabu Msaidizi,Dereva wa Ambulance na Katibu Muhtasi. October 12, 2021
  • TENDER MVOMERO May 28, 2022
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RUWASA MVOMERO YAPONGEZWA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI KWA UFANISI

    April 13, 2025
  • MWENGE WA UHURU KUMULIKA MIRADI YA MAENDELEO 7 YENYE THAMANI YA TSH. 1.06 WILAYANI MVOMRO

    April 13, 2025
  • DC MVOMERO AAGIZA SHULE SHIKIZI MINGO ISAJILIWE, IPOKEE WANAFUNZI JANUARI 2025

    March 27, 2025
  • KUU MVOMERO YAKISHUKURU KIWANDA CHA SUKARI MTIBWA KWA KUSAIDIA WANANCHI KURUDISHA MTO KWENYE MKONDO WAKE

    March 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kimkoa yafanyika Halimashauri ya Wilaya Mvomero
Video Zaidi

Viungo vya Haraka

  • Ukurasa wa Facebook

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais Ikulu
  • Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira
  • Baraza la Mtihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero

    Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO

    Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348

    Mobile: +255 23 293 4348

    Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani Eneo
    • Huduma

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.