Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Ndg. Paulo Faty amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika sekta ya afya na elimu, ambapo amesisitiza suala la ubora na matumizi sahihi ya fedha za Serikali katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo Julai 23, 2025 katika Kata ya Dakawa, Mkurugenzi huyo amesema miradi ya maendeleo inapaswa kutekelezwa kwa kuzingatia thamani halisi ya fedha (value for money), ubora wa kazi na kukamilika kwa wakati.
Katika sekta ya afya, Ndg. Paulo Faty amekagua ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali ya Wilaya, ujenzi wa Kituo cha Afya Dakawa na ukarabati wa zahanati ya kijiji cha Milama pamoja na ujenzi wa miundombinu ya maji safi ambayo inahusisha vyooo matundu matatu, kinawia mikono pamoja na shimo la majivu katika Zahanati ya Wami Dakawa.
Aidha, kwa upande wa sekta ya elimu, ametembelea ukarabati wa vyumba vitano vya madarasa na ujenzi ujenzi wa vyumba viwili vya viwili katika shule ya Msingi Msasani ambapo wananchi kwa kushirikiana na shirika la SAWA Wanawake Tanzania wamewezesha mradi huo.
Sambamba na hilo Mkurugenzi Mtendaji huyo amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali kwa kutoa ushirikiano katika miradi yote inayoletwa na Serikali na wadau wa maendeleo, akisema maendeleo ya kweli yanahitaji ushiriki wa wananchi.
Kwa upande wao, baadhi ya wananchi na viongozi wa vijiji walimpongeza Mkurugenzi huyo kwa kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi hiyo, wakisema hatua hiyo inawapa imani juu ya dhamira ya Serikali ya kuboresha maisha ya wananchi wa Mvomero.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.