Zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura limeanza rasmi tarehe 1 Machi,2025 katika Jimbo la Mvomero, huku wananchi wakionesha hamasa kubwa kushiriki na kupongeza utaratibu uliowekwa na Tume hiru ya Taifa ya Uchaguzi (iNEC).
Katika vituo vya Shule ya Msingi Dakawa na Kituo kilichopo Ofisi ya Kata ya Dakawa wananchi wameeleza kuridhishwa na utaratibu uliowekwa wa kuboresha taarifa zao.
Sambamba na hilo wananchi wahimizwa kujitokeza kwa wingi katika muda uliopangwa ili kuhakikisha wanaboresha taarifa zao na wale wanaostahili kuandikishwa wanafanya hivyo.
Zoezi la uboreshaji wa daftari litaendelea hadi tarehe 7 Machi, 2025 likilenga kuwahakikishia wananchi haki yao ya kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.