Wananchi 240,000 wilayani Mvomero wanatarajiwa kuandikishwa kwenye Orodha ya wapiga kura kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakao fanyika Novemba 27, 2024. Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Judith Nguli ametoa wito kwa wadau mbalimbali kushiriki kikamilifu katika kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuhakikisha kila mmoja anapata haki yake ya kidemokrasia.
Akizungumza Septemba 26, 2024 wakati akifungua kikao kazi kilicholenga kutoa maelekezo kuhusu uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa, DC Nguli amesema kuwa Wananchi 240000 wanatarajiwa kuandikishwa hivyo, ametoa wito kwa viongozi wa dini, Viongozi wa Wafugaji na wakulima, Viongozi wa vyama vya Siasa, Wasanii, Waandishi wa Habari, asasi za kiraia pamoja na viongozi wa mitaa kushirikiana na serikali katika kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kushiriki kikamilifu kwenye zoezi hili muhimu.
"...kila mtu kwa nafasi yake anatakiwa atusaidie kushawishi, akatusaidie kuhamasisha ili watu wakajiandikishe lakini mwisho wa siku wakapige kura..." amesema Mkuu wa Wilaya.
Wadau mbalimbali waliohudhuria kikao hicho waliunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa kila mwananchi anashiriki kwenye mchakato wa uchaguzi, wakisisitiza umuhimu wa elimu ya mpiga kura na ushirikishwaji wa jamii nzima.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.