• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
MVOMERO DISTRICT COUNCIL
MVOMERO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Afya
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Uongozi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Teknolojia,Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
    • Baraza la Madiwani
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Rasilimali Watu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Itakayo tekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Viwanda
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti

AHADI YA RAIS SAMIA KUHUSU BIMA YA AFYA KWA WOTE YAANZA KUTEKELEZWA, WASIMAMIZI VITUO VYA AFYA WAJENGEWA UWEZO KUFANIKISHA

Posted on: December 18th, 2025

Ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu 2025 kuhusu utekelezaji wa mpango wa Bima ya Afya kwa wote ndani ya siku 100 za mwanzo imeanza kuchukua sura mpya wilayani Mvomero, baada ya wasimamizi wa vituo vya kutolea huduma za afya, kujengewa uwezo ili kuhakikisha mpango huo unafanikiwa kwa ufanisi.


Mafunzo hayo maalumu yamefanyika Disemba 18, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero ambayo yamewakutanisha wasimamizi wa vituo vya afya, watoa huduma, Wajumbe wa timu ya Menejimenti ya Halmashauri (CMT) na Wajumbe wa Timu ya Usimamizi na uendeshaji wa Huduma za Afya (CHMT) Pamoja na wadau wa sekta ya afya wilayani humo.


Washiriki wa mafunzo hayo wamepatiwa elimu kuhusu namna bora ya kusimamia mfumo wa bima, utoaji wa huduma kwa wateja, usimamizi wa taarifa za afya, pamoja na mbinu za kupunguza changamoto zinazoathiri utekelezaji wa mpango huo.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Dkt. Phillipina Phillipo amesema kuwa utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote ni hatua muhimu katika kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wote bila ubaguzi, na kuongeza kuwa uelewa wa wasimamizi utaongeza ufanisi katika kutoa huduma stahiki.


Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA) Kanda Mashariki Bw. Zakaria Muyengi amesema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya utoaji wa elimu na hamasa kuhusu mpango na sheria ya Bima ya Afya kwa wote. Ameongeza kuwa lengo kuu la TIRA ni kuhakikisha kuwa watoa huduma za afya wanajisajili kwenye mfumo wa utambuzi wa ors.tira.go.tz.


Aidha, amebainisha kuwa mwitikio wa kujisajili na mfumo huo ni mzuri ambapo kati ya watoa huduma 91 wa Wilaya hiyo watoa huduma 70 wameshajiandikisha huku 21 pekee bado hawajajisajili, pia ametoa wito kwa wananchi kujiunga na bima.


Naye Dkt. Sami Haruna kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ameeleza matarajio yao ni kupata wanachama wengi huku akitoa rai kwa vituo vya kutolea huduma za afya kujiandaa vizuri

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 14, 2025
  • MAJINA YA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WALIOITWA KWENYE USAILI OKTOBA 17, 2025 October 14, 2025
  • MAJINA YA RESERVE WA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WANAOTAKIWA KWENYE USAILI KATIKA KATA October 14, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DC DOTTO AZUIA ENEO LA KIJIJI LILILOUZWA KINYUME NA UTARATIBU, AAGIZA ALIYENUNUA ARUDISHIWE FEDHA ZAKE

    December 18, 2025
  • AHADI YA RAIS SAMIA KUHUSU BIMA YA AFYA KWA WOTE YAANZA KUTEKELEZWA, WASIMAMIZI VITUO VYA AFYA WAJENGEWA UWEZO KUFANIKISHA

    December 18, 2025
  • DC MVOMERO ATOA SIKU SABA WAFUGAJI WALIOVAMIA SKIMU YA UWAWAKUDA KUONDOLEWA

    December 17, 2025
  • HISTORIA YAANDIKWA: WANANCHI WAPATA GARI LA WAGONJWA, WAISHUKURU SERIKALI KUWAONDOLEA ADHA KUSAFIRISHA WAGONJWA WA RUFAA

    December 16, 2025
  • Tazama Zote

Video

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kimkoa yafanyika Halimashauri ya Wilaya Mvomero
Video Zaidi

Viungo vya Haraka

  • Ukurasa wa Facebook

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais Ikulu
  • Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira
  • Baraza la Mtihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero

    Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO

    Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348

    Mobile: +255 23 293 4348

    Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani Eneo
    • Huduma

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.