• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
MVOMERO DISTRICT COUNCIL
MVOMERO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Afya
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Uongozi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Teknolojia,Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
    • Baraza la Madiwani
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Rasilimali Watu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Itakayo tekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Viwanda
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti

DC DOTTO AZUIA ENEO LA KIJIJI LILILOUZWA KINYUME NA UTARATIBU, AAGIZA ALIYENUNUA ARUDISHIWE FEDHA ZAKE

Posted on: December 18th, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mhe. Maulid Dotto, amezuia rasmi uuzaji wa eneo la kijiji lililopo katika Kitongoji cha Majengo, Kata ya Mlali ambapo imebainika kuwa eneo hilo limeuzwa kinyume na taratibu za kisheria, na kutoa agizo kwa uongozi wa kijij cha Kipera kuhakikisha mnunuzi wa eneo hilo anarudishiwa fedha zake mara moja.


Agizo hilo ametoa Disemba 18, 2025 kwenye mkutano wa kijiji hicho, ambapo wananchi wametoa taarifa juu ya uuzaji holela wa ardhi ya kijiji bila kufuata kanuni za usimamizi wa ardhi, na bila kupata ridhaa ya mkutano mkuu wa kijiji kama sheria inavyoelekeza.


Akizungumza mbele ya wananchi, Mhe. Dotto ameeleza kuwa ardhi ya kijiji haiwezi kuuzwa kiholela na mtu au kikundi cha watu, bali maamuzi lazima yafanywe na serikali ya kijiji kwa kushirikisha mkutano mkuu. Ameongeza kuwa ametoa agizo kwa Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya kufanya uchunguzi ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa wale watakaobainika kuhusika kwenye mpango huo.


“…nimesitiza uuzaji huo na fedha zilizolipwa kwa ajili ya eneo hilo zirudi kwa mwenyewe…” amesema Mkuu wa Wilaya.


Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi kuendelea kuchangia fedha za ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Kipera ambapo ujenzi wake umefikia hatua ya lent ana tayari Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha kiasi cha shilingi milioni 50 kwa ajili ya hatua ya umaliziaji wa Zahanati hiyo.


Wananchi wa kijiji hicho waliipongeza serikali ya wilaya kwa hatua hiyo, wakisema imekuja wakati muafaka kutokana na matukio ya mara kwa mara ya baadhi ya viongozi na watu binafsi kuuza ardhi kinyume cha utaratibu


MWISHO.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 14, 2025
  • MAJINA YA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WALIOITWA KWENYE USAILI OKTOBA 17, 2025 October 14, 2025
  • MAJINA YA RESERVE WA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WANAOTAKIWA KWENYE USAILI KATIKA KATA October 14, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DC DOTTO AZUIA ENEO LA KIJIJI LILILOUZWA KINYUME NA UTARATIBU, AAGIZA ALIYENUNUA ARUDISHIWE FEDHA ZAKE

    December 18, 2025
  • AHADI YA RAIS SAMIA KUHUSU BIMA YA AFYA KWA WOTE YAANZA KUTEKELEZWA, WASIMAMIZI VITUO VYA AFYA WAJENGEWA UWEZO KUFANIKISHA

    December 18, 2025
  • DC MVOMERO ATOA SIKU SABA WAFUGAJI WALIOVAMIA SKIMU YA UWAWAKUDA KUONDOLEWA

    December 17, 2025
  • HISTORIA YAANDIKWA: WANANCHI WAPATA GARI LA WAGONJWA, WAISHUKURU SERIKALI KUWAONDOLEA ADHA KUSAFIRISHA WAGONJWA WA RUFAA

    December 16, 2025
  • Tazama Zote

Video

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kimkoa yafanyika Halimashauri ya Wilaya Mvomero
Video Zaidi

Viungo vya Haraka

  • Ukurasa wa Facebook

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais Ikulu
  • Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira
  • Baraza la Mtihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero

    Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO

    Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348

    Mobile: +255 23 293 4348

    Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani Eneo
    • Huduma

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.