• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
MVOMERO DISTRICT COUNCIL
MVOMERO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Afya
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Uongozi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Teknolojia,Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
    • Baraza la Madiwani
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Rasilimali Watu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Itakayo tekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Viwanda
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti

WITO UMETOLEWA KWA WADAU, SERIKALI KUONGEZA JUHUDI KATIKA UTOAJI ELIMU YA HEDHI SALAMA VIJIJINI

Posted on: May 28th, 2025

Wito umetolewa kwa Serikali pamoja na wadau wa maendeleo kuongeza juhudi katika utoaji wa elimu ya hedhi salama kwa watoto wa kike walioko vijijini, ili kusaidia kuondoa changamoto wanazokutana nazo wakati wa kipindi chao cha hedhi.

Wito huo umetolewa Mei 28, 2025 na Afisa Tawala Wilaya ya Mvomero Bw. Flezier Mang’ula akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo katika maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.

Afisa Tawala huyo amesema kuwa bado kuna uelewa mdogo kuhusu hedhi salama katika maeneo ya vijijini, ambako miradi ya kuwasaidia wasichana kutoka na hedhi haipo, hali inayosababisha aibu, unyanyapaa na hata utoro mashuleni kwa wasichana.

"…ziko jitihada zinazohitajika kwa Serikali kwa maana ya Halmashauri kwa kushirikiana na wadau ili kuweza kutoa elimu ya kuwasaidia wananchi na wanafunzi kufikia hedhi salama…” amesema Bw. Mang’ula.

Aidha, amelipongeza shirika la AfriCraft kupitia mradi wao wa Binti ambao unatoa elimu na mafunzo ya utengenezaji wa taulo za kike za kufua kwa wanafunzi na walimu wa Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA DAKAWA, VETA KIHONDA) Pamoja na shule za sekondari za Mvomero, Sokoine Memorial na Wami Dakawa.

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Dkt. Phillipina Phillipo amesema Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya shule ambapo inajenga vyoo vyenye vyumba maalum kwa ajili ya wasichana kujisitili wakati wa hedhi pamoja na kutoa taulo za kike za kisasa kwa kila shule.

Kwa upande wake, Meneja Miradi ya Afya kutoka Shirika la AfriCraft ambalo linatekeleza mradi wa Binti Bi. Aneth Kiyao amesema kuwa hadi sasa wamefanikiwa kuwafikia wasichana zaidi ya 35000 ambao wamepatiwa taulo za kike, Wavulana 18000 ambao wamepatiwa elimu ya hedhi na usawa wa kijinsia.

Akizungumza kwa niaba ya wasichana waliopata elimu na mafunzo juu ya hedhi salama, Mwanafunzi Anastazia Sunday kutoka shule ya Sekondari Mvomero amesema kupitia mradi huo umesaidia kupunguza utoro kwa wasichana ambao walikuwa hawafiki shule wakati wa hedhi.

Matangazo

  • MAJINA YA WAANDISHI WASAIDIZI NA BVR KIT OPERATORS. February 22, 2025
  • Majina ya Waandishi wasaidizi na BVR KIT Operators February 22, 2025
  • Kuitwa Kwenye Usahili Nafasi Ya Mtendaji Wa Kijiji,Mtunza Kumbukumbu,Afisa Hesabu Msaidizi,Dereva wa Ambulance na Katibu Muhtasi. October 12, 2021
  • TENDER MVOMERO May 28, 2022
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WITO UMETOLEWA KWA WADAU, SERIKALI KUONGEZA JUHUDI KATIKA UTOAJI ELIMU YA HEDHI SALAMA VIJIJINI

    May 28, 2025
  • WAHE. MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MLIMBA WATEMBELEA MVOMERO KUJIFUNZA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI UNAVYOWAKOMBOA WAKULIMA WA KAKAO

    May 24, 2025
  • MVOMERO KUUZA UFUTA KUPITIA STAKABADHI GHALANI KUANZIA MEI 20, 2025

    May 16, 2025
  • MKURUGENZI INEC AWASISITIZA WAANDHISHI WASAIDIZI, WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI NGAZI YA KITUO KUZINGATIA MUDA WA KUFUNGUA VITUO VYA KUANDIKISHA WAPIGA KURA

    May 14, 2025
  • Tazama Zote

Video

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kimkoa yafanyika Halimashauri ya Wilaya Mvomero
Video Zaidi

Viungo vya Haraka

  • Ukurasa wa Facebook

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais Ikulu
  • Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira
  • Baraza la Mtihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero

    Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO

    Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348

    Mobile: +255 23 293 4348

    Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani Eneo
    • Huduma

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.