Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa ameitaka Jamii kuwa na utaratibu wa kupima maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU), ili kujua hali ya Afya zao na kuweza kuendelea kujiimarisha kwa namna mbalimbali.
Hayo ameyasema Desemba Mosi 2023 katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika viwanja vya Shule ya Sekondari Morogoro iliyoko Mjini Morogoro.
Aidha, Mhe.Kassim Majaliwa ameainisha matokeo ya tafiti za maswala ya UKIMWI zinazoonesha kuwa wanawake wako mstari wa mbele katika upimaji ukilinganisha na wanaume, hali ambayo inasababisha wanawake kutumia dawa na kufubaza virusi vya UKIMWI pale wanapobainika ni waathirika wa ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa tafiti hizo, vijana wengi hasa wa kike wanamaambukizi ya VVU ukilinganisha na watu wazima pamoja na wazee.
Hata hivyo, lengo la maadhimisho hayo UKIMWI ni pamoja na Jamii kujitathmini ilipotoka, ilipo na inapoelekea katika Afua za UKIMWI, lakini pia kutoa Elimu ya kupambana na UKIMWI, kutoa faraja kwa wajane na watoto yatima waliotokana na kupoteza ndugu na jamaa zao kwa UKIMWI, kuangalia namna gani Serikali inaratibu mipango endelevu katika kuondoa maambukizi mapya ya VVU kumaliza vifo vitokanavyo na UKIMWI sambamba na kutokomeza unyanyapaa kwa waishio na UKIMWI ili kufikia lengo la 000 ifikapo Mwaka 2030.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.