Katibu Tawala Wilaya ya Mvomero Bw. Said Nguya amewataka watumishi wa Halmashauri hiyo kujitoa kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii kwani uimara wa mtu kwenye kazi upimwa na kwa ushiriki wake katika shughuli za kijamii.
Bw. Nguya ametoa kauli hiyo Aprili 24, 2024 wakati wa mazoezi ya viungo ikiwa ni miongoni mwa shughuli zinazofanyika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Katibu Tawala huyo amesema kufanya kazi kwa bidii hakumfanyi mtu kuwa bora kwenye kila kitu bali kujitoa kushiriki shughuli za kijamii kama vile michezo umuongezea mtu ufanisi katika utumishi wake.
“…kama kuna michezo shirikiana na wenzako kama kuna shughuli zingine zipo kwa mujibu wa ratiba kushirikiana ni sehemu ya kupima uwajibikaji wako…” amesema Katibu Tawala.
Aidha, Bw. Said Nguya ameendelea kuwasisitiza watumishi na wananchi Wilayani humo kushiriki katika matukio yanayoendelea kufanyika Wilayani humo kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.