Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero wakiwemo Madiwani, Wakuu wa Idara na Watumishi wametakiwa kushikamana kwa kufanya kazi kwa umoja kwa lengo la kuinua Halmashauri hiyo na kuacha mifarakano ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya Wilaya hiyo.
Hayo yamesemwa Mei 8, 2024 na Mwenyekiti wa Hamlashauri hiyo Mhe. Yusuph Makunja wakati akifungua mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Mhe. Makunja amewataka Waheshimiwa Madiwani kushikamana na wenzao ili kuhakikisha kuwa maendeleo ya Wilaya hiyo yanafikiwa kwa wakati. Aidha, amewasisitiza kuheshimiana pamoja na kutii maelekezo ya Serikali.
“...tuheshimiane, tuheshimu Serikali, tuheshimu vikao…” amesema Mwenyekiti.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo amewakumbusha Watumishi wa Halmashauri pamoja na Madiwani kutimiza wajibu wao na kwamba uwepo wao si kwa ajili ya Mvomero pekee bali ni makusudi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.