Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata wametakiwa kuzingatia hatua, miongozo na taratibu zote za kisheria katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ili kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa haki, amani na kwa kuzingatia misingi ya demokrasia.
Wito huo umetolewa na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo Bw. Amos Kanige wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata yaliyofanyika katika ukumbi wa Prof. Kuzilwa uliyopo katika Kata ya Mzumbe.
Bw. Kanige amesema kuwa Uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali za kikatiba na kisheria ambazo upaswa kufuatwa na kuzingatiwa huku akiongeza kuwa hatua na taratibu hizo ndiyo msingi wa Uchaguzi bora na wenye ufanisi na kupunguza ama kuondoa kabisa malalamiko au vulugu wakati wote wa uchaguzi.
"...natumia fursa hii kuwaasa kuwa pamoja na uzoefu ambao baadhi yenu mnao katika uendeshaji wa Uchaguzi msiache kusoma katiba, sheria kanuni, taratibu, miongozo na fuateni na kutekeleza maelekezo mbalimbali yatakayotolewa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)..." amesema Bw. Kanige.
Aidha, amewakumbusha wasimamizi hao kuwa wanabeba dhamana kubwa katika kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kwa weledi, wakizatia kuwa nafasi waliyopewa ni ya kuaminika na nyeti, hivyo wanapaswa kuzingatia maadili na uadilifu wakati wote wa mchakato wa uchaguzi.
Ikumbukwe kuwa Uchaguzi Mkuu huo utafanyika Oktoba 29, 2025 hivyo wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wao ambapo Uchaguzi huu utahusisha kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani.
"Kura yako, Haki yako, Jitokeze kupiga kura".
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.