Afisa Muandikishaji Daftari la kudumu la wapiga kura Jimbo la Mvomero Bi. Mary Kayowa amewapongeza wananchi wanaoendelea kujitokeza Kujiandikisha au kuboresha taarifa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura katika maeneo mbalimbali Wilayani Mvomero.
Bi. Mary Kayowa ametoa pongezi hizo Machi 4, 2025 alipotembelea vituo mbalimbali vya kuandikisha wapiga kura katika kata za Dakawa, Mzumbe, Mangae na Doma ambapo amekuta wananchi wamejitokeza Kujiandikisha au kuboresha taarifa zao.
Pamoja na pongezi hizo, amewataka kwenda kuwahamasisha wananchi wengine ambao bado hawajajiandikisha kujitokeza ili waweze kuboresha taarifa zao kabla ya tarehe 7 Machi, 2025 ambapo ni mwisho wa zoezi hilo la uboreshaji.
Vituo alivyotembelea Afisa Muandikishaji huyo ni pamoja na kituo kilichopo ofisi ya mtendaji kata ya Dakawa, Shule ya msingi Wami Dakawa, Kituo cha stendi ofisi ya mtendaji wa Kijiji Sangasanga, Shule ya Msingi Changarawe, Shule ya sekondari Mzumbe, ofisi ya kata za Doma na Mangae.
"Kujiandikisha kuwa Mpiga kura ni msingi wa Uchaguzi Bora".
MWISHO
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.