Mwenge wa Uhuru 2024 umewapongeza wananchi wa Kijiji cha Kunke kwa kuchangia maendeleo ikiwemo ujenzi wa zahanati ya Kijiji hicho ambapo imeelezwa kuwa wananchi hao wamechangia zaidi ya milioni 20 ili kufanikisha ujenzi wa Zahanati hiyo.
Pongezi hizo zimetolewa Aprili 20, 2024 na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 Ndg. Godfrey Eliakimu Mzava wakati akiweka jiwe la msingi katika jengo la Zahanati hiyo iliyopo katika Kijiji cha Kunke Wilayani Mvomero.
Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge amesema utayari wa wananchi hao katika kuchangia ujenzi wa Zahanati hiyo unaonesha ni jinsi gani walivyo na uhitaji wa huduma za jamii ikiwemo huduma za Afya.
“…tunawapongeza sana wananchi wa eneo hili kwa utayari wao kwa ajili ya ujenzi huu…” amesema Ndg. Godfrey Mzava.
Sambamba na hilo Ndg. Mzava ameisisitiza Halmashauri ya Mvomero kusimamia ukamilishaji wa Zahanati hiyo ili wananchi wa eneo hilo waanze kupata huduma za Afya.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.