Wakulima wa zao la mpunga Wilayani Mvomero wameshauriwa kutumia mbegu bora na zenye zinatija ya uzalishaji ambazo zimefanyiwa utafiti na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo TARI ili kuongeza uzalishaji na kukuza vipato vyao.
Ushauri huo umetolewa Julai 22, 2024 na Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmasahuri ya Wilaya ya Mvomero Bw. Mohamed Longoi kwenye siku ya Mkulima shambani iliyoandaliwa na TARI katika Kijiji cha Mbogo kilichopo Wilayani humo.
Bw. Longoi amebainisha kuwa kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi hivyo wakulima hawanabudi kubadilisha mfumo wa uzalishaji wa zao hilo ili kuendana na mahitaji ya soko.
"...usipande ilimrdadi mbegu, panda mbegu bora..." amesema Afisa Kilimo.
Aidha, amewataka wakulima kushirikiana na wataalam wa kilimo, Taasisi, Serikali, Mashirika ya Umma na wadau mbalimbali ambao wanamchango chanya katika kukuza sekta ya kilimo.
Sambamba na hilo, Afisa Kilimo huyo amesema baadhi ya wakulima wamekuwa na mwitikio chanya kwenye ufuatiliaji wa kilimo cha kisasa ambacho kina ongeza uzalishaji wa zao hilo.
Naye, Mtafiti wa Kilimo kutoka TARI kituo cha Dakawa Bi. Fabiola Langa amesema Taasisi ya TARI Dakawa imejikita katika kutafiti wa kugundua mbegu bora za mpunga na Teknolojia mbalimbali za kilimo ambazo zinaongeza tija kwa wakulima na wadau hususan kwenye zao la mpunga.
Bi. Fabiola ameongeza kuwa hadi sasa wamegundua mbegu bora za mpunga zaidi ya 20 ambazo tayari zimethibitishwa kwa kutumiwa na wakulima. Akitolea mfano wa mbegu ya 'SARO FIVE' ameeleza kuwa mbegu hiyo inapendwa na wakulima pamoja na wadau wa mpunga kutokana na kuongeza tija ya uzalishaji na kipatao kwa wakulima.
Nao wakulima wa zao la mpunga katika Skimu ya Umwagiliaji ya Mbogo kwa Mtonga akiwemo Bw. Ally Palainda ameishukuru TARI kwa kuwapatia mafunzo na mbegu bora ambazo zitawasaidia kuongeza uzalishaji. Pia ameiomba Serikali kuwwajengea miundombinu bora ya Umwagiliaji kutokana na skimu hiyo kuwa ya kienyeji ambapo wamekuwa wakipata changamoto hususan wakati wa mvua ambayo uharibu miundombinu yao.
Skimu ya Umwagiliaji ya Mbogo kwa Mtonga ina zaidi ya ekari 9500 huku ikiwa na wakulima ziadi ya 9000.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.