Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero likiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mhe. Yusuph Makunja wamejadili na kupitisha bajeti ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kiasi cha shilingi bilioni 59,464,950,810
Akiwasilisha mpango wa bajeti hiyo mbele ya Baraza la Madiwani, Afisa Mipango na Uratibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Bw. Amos Kanige amesema kuwa Halmashauri inakisia kukusanya jumla ya shilingi Bilioni 59,464,950,810 kutoka vyanzo vya mapato vya Halmashauri hiyo, Ruzuku ya Serikali kuu na Wadau wa Maendeleo.
Aidha, ameongeza kuwa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri, wanakisia kukusanya kiasi cha bilioni 5,556, Ruzuku ya Serikali kuu kiasi cha bilioni 49 na fedha kutoka kwa wadau wa maendeleo ni kiasi cha bilioni 4,865.
Sambamba na hilo, Afisa Mipango huyo amebainisha vipaumbele vya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2025/2026 vikiwemo, kuboresha huduma za elimu kwa kutoa elimu bila malipo kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha sita, kuboresha miundombinu ya elimu, kuboresha huduma za Afya, kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri, kuwezesha wananchi kiuchumi na kuendelea kutoa ruzuku ya kunusuru kaya maskini kupitia mpango wa TASAF III.
Akizungumza baada ya kupitishwa kwa bajeti hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Bi Loema Peter amewashukuru Waheshimiwa Madiwani pamoja na Mkuu wa Wilaya kwa kuridhia na kupitisha bajeti ya Halmashauri pamona na bajeti ya TARURA.
MWISHO
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.