Waheshimiwa Madiwani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Mei 24, 2025 wamefanya ziara ya mafunzo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kwa lengo la kujifunza namna mfumo wa Stakabadhi ya Mazao Ghalani unavyotekelezwa na kusaidia kuwawezesha wakulima wa zao la kakao kupata manufaa makubwa kupitia mfumo huo.
Katika ziara hiyo, madiwani hao wametembelea Kitalu cha kuzalisha miche ya kakao kilichopo katika Kata ya Mhonda pamoja na ghala la linalotumiwa kuhifadhi kakao na kujionea namna kakao inavyopokelewa, kupimwa ubora, kuhifadhiwa na baadaye kuuzwa kupitia minada ya ushindani ambayo huwapatia wakulima bei nzuri zaidi tofauti na mfumo wa kawaida wa uuzaji wa mazao.
Akizungumza katika ziara hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mvomero Mhe. Christopher Maarifa amesema kuwa mfumo huo umeonekana kuwa na faida kubwa kwa wakulima wa Mvomero ambapo kabla ya mfumo huo walikuwa wakiuza kwa shilingi 2000 kwa kilo, baada ya kuanza kutumia mfumo huo bei imepanda hadi kufikia elf 29,000 kwa kilo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Mhe. Innocent Mwangasa kwa niaba ya Madiwani wa Mlimba ameeleza kufurahishwa na elimu waliyoipata na kuahidi kwenda kuishirikisha jamii pamoja na kuhimiza wakulima kuendelea kuutumia mfumo wa Stakabadhi ghalani.
Aidha, amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima kwa kuwa msatari wa mbele kuhamasisha wananchi kujikita katika kuzalisha mazao ya kimkakati likiwemo zao la kakao.
MWISHO
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.