Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mh. Mohamedi Utaly leo amemkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. Florent Kyombo jumla ya Vitambulisho elfu kumi (10,000) kwa aili ya kugawa kwa wafanya biashara wadogo (wajasiriamali) walioko katika wilaya hiyo.
Akizungumzamara baada ya kukabidhi vitambulisho hivyo kwenye kiao maalum kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo, amesema ni muhimu kila Mtendaji wa kata au kijiji kulichukulia kwa umuhimu wa aina yake zoezi hilo ili kuhakikisha vitambulisho hivyo vitagawiwa kwa walengwa waliokusudiwa.
Akipokea vitambulisho hivyo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji amesema atahakikisha anasimamia zoezi hilo kwa umakini mkubwa na kuvigawa kwa walengwa waliokusudiwa bila ubaguzi wa aina yoyoyte ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa ya Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Ndug. Florent Kyombo akitoa maelekezo kwa watendaji wa vijiji na kata juu ya ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali wadogo
Meneja wa TRA Wilayani Mvomero akieleza kwa watendaji wa kata na vijiji juu ya sifa za wajasiriamali wanaostahili kupewa vitambulisho vya wajasiriamali wadogo.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.