Kikao cha Kamati ya ushauri Wilaya (DCC) chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Maulid Dotto ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero kimeketi kwa ajili ya kujadili na kupitisha Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri, Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA), Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa mwaka wa fedha 2026/2027.



Kikao hicho kimefanyika Februari 12, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kikiwakutanisha wajumbe kutoka makundi mbalimbali.
Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya amewasisitiza watumishi wote pamoja na viongozi wanaendelea kushirikiana ili kuhakikisha kuwa malengo ambayo halmashauri imejiwekea ya kutoa huduma bora kwa wananchi yanafikiwa.



Aidha, ametoa wito kuwahamasisha wananchi kulima mazao ya kimkakati kama vile kokoa na karafuu ili yawainue kiuchumi. Pia ameendelea kuhimiza wananchi kujiunga na mpango wa Bima ya Afya kwa wote.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mhe. Koila Majuka kwa niaba ya Baraza la Madiwani ameeleza kuwa watashirikiana kwa karibu na Taasisi za TARURA na RUWASA ili kuhakikisha kuwa zinapata fedha za kutekeleza miradi kwa kuwa maji na barabara ni vichocheo muhimu vya maendeleo ya wananchi.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Ndg. Paulo Faty amemhakikishia Mkuu wa Wilaya kuwa maelekezo na ushauri uliotolewa na wajumbe.






MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.