• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
MVOMERO DISTRICT COUNCIL
MVOMERO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Afya
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Uongozi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Teknolojia,Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
    • Baraza la Madiwani
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Rasilimali Watu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Itakayo tekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Viwanda
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti

SERIKALI YACHUKUA HATUA KUTATUA MGOGORO WA ARDHI KIJIJI CHA DOMA, DC DOTTO ATAKA WANANCHI WALIO KATIKA ENEO LA MGOGORO KUTAMBULIWA

Posted on: February 11th, 2026

Serikali ya Wilaya ya Mvomero imeanza kuchukua hatua madhubuti za kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu katika Kijiji cha Doma, kwa lengo la kurejesha amani, mshikamano na haki kwa wananchi.


Hatua hiyo imeelezwa Februari 11, 2026 na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mhe. Maulid Dotto, wakati wa kikao maalum kilichofanyika kijijini hapo, kilichowakutanisha viongozi wa kijiji, wananchi na wataalamu kutoka sekta ya ardhi.


Mhe. Dotto amesema kuwa serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha mgogoro huo unamalizika kwa njia ya haki na kwa kuzingatia sheria, taratibu na maslahi ya wananchi wote.


Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya, amesisitiza umuhimu wa kuwatambua rasmi wananchi wote waliopo katika eneo la mgogoro, ili kuwezesha serikali kupata takwimu sahihi zitakazosaidia katika upangaji na utoaji wa maamuzi ya kudumu. Ameongeza kuwa zoezi hilo litahusisha uhakiki wa umiliki wa ardhi, mipaka ya shamba pamoja na nyaraka halali za umiliki.


Kwa upande wake, Afisa Ardhi wa Wilaya Bw. Charles Wandwi ameeleza kuwa timu ya wataalamu ipo tayari kufanya kazi ya uhakiki wa maeneo husika, huku wananchi wakihimizwa kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa sahihi na kujitokeza wakati wa zoezi hilo.


Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mhe. Koila Majuka ameelza kuwa Waheshimiwa Madiwa kwa kushirikiana na Timu ya Mkuu wa Wilaya watahakikisha wananchi wanapata haki yao Pamoja na mwenyekezaji naye anapata haki yake.


Diwani wa Kata hiyo ya Doma amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuchukua hatua ya kutatua mgogoro huo huku akisisitiza kuwa zoezi la uhakiki lifanyike kwa uwazi.


Wananchi wa Kijiji cha Doma wameishukuru serikali kwa kuchukua hatua za haraka na kuahidi kushirikiana kikamilifu katika zoezi la utatuzi wa mgogoro huo, wakieleza matumaini yao kuwa suluhisho la kudumu litapatikana na kuondoa migogoro ya mara kwa mara iliyokuwa ikikwamisha maendeleo ya kijiji hicho.


MWISHO.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 14, 2025
  • MAJINA YA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WALIOITWA KWENYE USAILI OKTOBA 17, 2025 October 14, 2025
  • MAJINA YA RESERVE WA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WANAOTAKIWA KWENYE USAILI KATIKA KATA October 14, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WAANDAAJI WA MAUDHUI MTANDAONI WILAYA YA MVOMERO WAJITOKEZA KUCHANGAMKIA FURSA

    February 13, 2026
  • RAIS SAMIA ALIAHIDI NA AMETEKELEZA: WANANCHI 9,254 MVOMERO KUNUFAIKA BIMA YA AFYA KWA WOTE AWAMU YA KWANZA

    February 13, 2026
  • KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI WILAYA (DCC)

    February 12, 2026
  • SERIKALI YACHUKUA HATUA KUTATUA MGOGORO WA ARDHI KIJIJI CHA DOMA, DC DOTTO ATAKA WANANCHI WALIO KATIKA ENEO LA MGOGORO KUTAMBULIWA

    February 11, 2026
  • Tazama Zote

Video

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kimkoa yafanyika Halimashauri ya Wilaya Mvomero
Video Zaidi

Viungo vya Haraka

  • Ukurasa wa Facebook

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais Ikulu
  • Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira
  • Baraza la Mtihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero

    Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO

    Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348

    Mobile: +255 23 293 4348

    Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani Eneo
    • Huduma

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.