• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
MVOMERO DISTRICT COUNCIL
MVOMERO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Afya
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Uongozi
      • Usafi na Mazingira
      • Ujenzi
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
    • Vitengo
      • Teknolojia,Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
    • Baraza la Madiwani
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Rasilimali Watu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Itakayo tekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Viwanda
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti

RAIS SAMIA ALIAHIDI NA AMETEKELEZA: WANANCHI 9,254 MVOMERO KUNUFAIKA BIMA YA AFYA KWA WOTE AWAMU YA KWANZA

Posted on: February 13th, 2026

Wananchi wapatao 9,254 wa Wilaya ya Mvomero wanatarajia kunufaika na mpango wa Bima ya Afya kwa Wote katika awamu ya kwanza, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoitoa wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika Oktoba 29, 2025.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa zoezi la uhakiki, usajili na ugawaji wa kadi za bima iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri Februari 13, 2026, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Ndg. Said Nguya amesema mpango huu ni sehemu ya jitihada za Serikali kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora za afya bila vikwazo vya kifedha huku akieleza kuwa mpango huu unalenga kuwafikia wananchi wote, hususan wa kipato cha chini, ili kuimarisha ustawi wa jamii.

 Kwa upande wake, Afisa Uanachama Mwandamizi kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Morogoro Bi. Rosemilia Msigwa amebainisha kuwa kwa Wilaya ya Mvomero pekee jumla ya Kaya 2,106 zenye wakazi 9,254 zitasajiliwa na kupatiwa kadi za bima kwa awamu ya kwanza akiongeza kuwa Serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni 315,900,000 kwa ajili ya bima. Aidha, ameongeza kuwa Bima hiyo itawawezesha kupata huduma katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya Serikali.

Naye, Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt. Phillipina Phillipo ameeleza kuwa Idara ya Afya imejipanga kuwapokea na kuwahudumia wanachama wapya wa bima ya Afya, akiongeza kuwa maandalizi yamefanyika ikiwemo ya kuboresha huduma kwa kuongeza watoa huduma, vifaa tiba Pamoja na kusajili vituo vyote katika mfumo wa bima unaoratibiwa na Mamlaka ya usimamizi wa bima Tanzania – TIRA.

Nao, wananchi waliopatiwa bima hiyo wameeleza kufurahishwa na hatua hiyo, wakisema itapunguza gharama za matibabu na kuwawezesha kupata huduma kwa wakati, wakiongeza kuwa awali walikuwa wakikumbwa na changamoto ya kugharamia matibabu, hali iliyokuwa ikiathiri maisha yao na familia zao.

 MWISHO.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 14, 2025
  • MAJINA YA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WALIOITWA KWENYE USAILI OKTOBA 17, 2025 October 14, 2025
  • MAJINA YA RESERVE WA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA WANAOTAKIWA KWENYE USAILI KATIKA KATA October 14, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WAANDAAJI WA MAUDHUI MTANDAONI WILAYA YA MVOMERO WAJITOKEZA KUCHANGAMKIA FURSA

    February 13, 2026
  • RAIS SAMIA ALIAHIDI NA AMETEKELEZA: WANANCHI 9,254 MVOMERO KUNUFAIKA BIMA YA AFYA KWA WOTE AWAMU YA KWANZA

    February 13, 2026
  • KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI WILAYA (DCC)

    February 12, 2026
  • SERIKALI YACHUKUA HATUA KUTATUA MGOGORO WA ARDHI KIJIJI CHA DOMA, DC DOTTO ATAKA WANANCHI WALIO KATIKA ENEO LA MGOGORO KUTAMBULIWA

    February 11, 2026
  • Tazama Zote

Video

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kimkoa yafanyika Halimashauri ya Wilaya Mvomero
Video Zaidi

Viungo vya Haraka

  • Ukurasa wa Facebook

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma
  • Ofisi ya Rais Ikulu
  • Ofisi ya Rais Tamisemi
  • Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira
  • Baraza la Mtihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero

    Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO

    Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348

    Mobile: +255 23 293 4348

    Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani Eneo
    • Huduma

Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.