Wakulima wadogo Wilayani Mvomero wametakiwa kutumia fursa ya kilimo cha mazao ya matunda na mbogamboga, pamoja na ufugaji wa kisasa ili kuongeza kipato na kukuza mnyororo wa thamani kwa ajili ya kuboresha kipato na maisha kwa ujumla.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Bi. Natujwa Mellau wakati wa uzinduzi wa mradi wa uwezeshaji wa mbinu bunifu kwa wakulima wadogouliofanyika hapo jana katika ukumbi wa Halmashauri na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa kilimo wilayani humo.
Kaimu Mkurugenzi huyo amesema kuwa ni vyema wakulima wadogo wakatumia fursa hiyo ya mradi kuongeza kipato chao kwa kulima na kufuga kwa kutumia utaalamu watakaoupata ili kuongeza tija katika ufanisi wa shughuli zao za uzalishaji.
Naye Afisa Mradi Bw. Pius Ngirwa amesema wameamua kutanua mradi na kuuleta katika Wilaya ya Mvomero kutokanana Wilaya hiyo kufanya vizuri katika baadhi ya maeneo ambayo walianza nayo yakiwemo vijiji vya Milama na Mvomerohivyo kuwahamasisha kuweza kuuleta mradi Wilayani Mvomero ili kuweza kupata walulima wengi Zaidi na kuboresha kipato kwa wakulima wadogo wilayani humo.
Aidha afisa Mradi huyo ameomba ushirikiano kwa uogozi wa Halamshauri kuanzia ngazi ya Wilaya mpaka vijijini wakati wa utekelezaji wa mradi ili kuweza kurahisisha utekelezaji na wananchi waweze kunufaika na mradi na kujiongezea kipato.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.