Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewapongeza Wataalam na Waheshimiwa Madiwani kwa ukusanyaji wa mapato yatokanayo na mnada na kueleza kuwa minada hiyo imekuwa ikichangia kiasi kikubwa katika mapato ya Halmashauri. Ameahidi kuwaleta wafugaji kutoka Wilaya nyingine ili waje kujifunza Mvomero. Halmashauri hiyo ina uwezo wa kukusanya zaidi ya Sh. Millioni 400 ndani ya mwaka mmoja badala ya kukusanya Shilingi Milioni 200 kutoka na minada. Aliipongeza Halmashauri kwa kukusanya kiasi cha Bilioni 3 sawa asilimia 96%.
Aliwataka wafugaji waache kuwasumbua wakulima kwa kufuga kisasa kwa kutengeneza zizi na kuchimba kisima kwa ajili ya mifugo yao. Aliwataka wafugaji wawe agenda ya kuibadilisha Mvomero.
Mkuu huyo wa Mkoa ameyasema hayo Juni 13 mwaka huu wakati wa Mkutano Maalum wa Baraza kujadili Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali – CAG uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo.
Akiongea katika Mkutano huo Mkuu wa Mkoa amewataka Madiwani watengeneze utaratibu wa kusimamia miradi katika maeneo yao. Aliwataka Wataalam wawashirikishe Wenyeviti wa Vijiji kwani ndio wenye miradi.
Pia alimtaka Mganga Mkuu wa Wilaya kuisimamia Hospitali ya Wilaya kwani ina changamoto ya wateja. Alimtaka kwenda kuangalia magonjwa yanayosumbua ndani ya Wilaya ili iwe Hospitali ya magonjwa maalum. Aliagiza kuundwa kwa Kamati Maalum ya madiwani ili iweze kusaidia kuitangaza Hospitali hiyo.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.