Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Ndg. Florent kyombo amewataka wananchi waliovamia eneo la hifadhi katika kijiji cha Mlumbilo, Mtibwa kuendelea kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa la kuwataka kuondoka katika eneo hilo na kutafuta maeneo mengine mbadala ya makazi.
Mkurugenzi Mtendaji ameyasema hayo hapo alipotembelea eneo hilo na kuzungumza na wananchi walioathirika na zoezi hilo.
Wakitoa kilio chao mbele ya Mkurugenzi, wananchi wamemuomba Mkurugenzi kuangalia uwezekano wa kuwatafutia eneo la kuishi kwani wengine wao baada ya kubomoa makazi yao hawana mahala pa kuishi na wanalazimika kuishi nje kama wanyama.
Mkurugenzi amewambia wananchi hao kwamba kutokana na maombi yao, atawasiliana na uongozi wa ngazi za juu ili kuangalia uwezekano huo , lakini pamoja na kupeleka maombi hayo amewataka wananchi hao kuendelea kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa la kuwataka kutoka katika eneo hilo mara moja hadi hapo maombi hao yatakaposhughulikiwa.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.