Katika kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mwl. Linno Mwageni ametoa wito kwa watumishi na wananchi wote kushiriki katika zoezi la upandaji miti ambalo litafanyika Desemba 7, 2024 huku akisema kuwa hatua hii si tu inalenga kuhifadhi mazingira bali pia ni ishara ya kudumisha urithi wa kizazi hiki na kusherehekea historia ya taifa kwa njia endelevu.
Mwl. Linno ametoa wito huo Desemba 6 mwaka huu wakati akizungumza na Watumishi wa Halmashauri pamoja na wananchi walioshiriki michezo iliyofanyika katika viwanja vya michezo vya Halmashauri hiyo kwa lengo la kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru.
Aidha, ameongeza kuwa kupanda miti ni hatua muhimu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuongeza uzuri wa maeneo yetu.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo amewapongeza Watumishi na wananchi waliojitokeza kushiriki katika michezo hiyo.
Michezo mbalimbali ilikuwepo ikiwemo jogging, mazoezi ya viungo, mpira wa miguu ambapo timu ya vijana wa usafi wameibuka na ushindi wa goli mbili kwa bila dhidi ya timu ya Halmashauri, kuvuta kamba na mpira wa pete.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.