Mamlaka ya Chakula na Dawa imetoa elimu kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Mvomero juu ya matumizi sahihi ya matumizi ya vyakula, vipodozi na madawa mbalimbali ili kulinda afya zao na kujiepusha kujiingiza kwenye mitego ya wafanyabiashara wasio waadilifu ambao nia yao ni kupata faida bila kujali afya za walaji.
Elimu hiyo ya ilitotolewa na watendaji wa TFDA kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Mvomero juma lililopita walipotembelewa wilayani humo kama moja ya jukumu lao kuelimisha umma juu ya madhara yatokanayo na matumizi mabovu ya bidhaa batili na kuwaasa wawe mabalozi wazuri kwa wananchi walioko vijijini na kokote wanapoenda.
Watendaji hao walionyesha mfano wa bidhaa za matumizi ya kila siku ambazo kwa mtu wa kawaida hawezi kugundua kama ni feki lakini kwa kuelimisha watafahamu kwamba bidhaa hizo ni feki na na hazifai kwa matumizi ya binadamu
 Akizungumza kwa niaba ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo Ndg. Florent Kyombo amewashukuru watendaji hao kwa kutoa elimu hiyo na kuwakaribisha tena kwa mara nyingine muda wowote na wajiskie wako nyumbani kwani elimu wanayotoa ni muhimu sana kwa afya za wananchi na taifa kwa ujumla
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.