Serikali kupitia Mpango wa kunusuru Kaya Maskini – TASAF imetoa kiasi cha shilingi 185,298, 000 kwa ajili ya kuwalipa walengwa 6130 wa mpango huo Wilayani Mvomero ambapo malipo hayo ni dirisha la mwezi Julai na Agosti, 2024.
Hayo yamebainishwa Novemba 07, 2024 na Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mahija Mdoe wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii ikiwa zoezi la ulipaji likiendelea kwa Vijiji 130 vya Wilaya hiyo.
Mratiu huyo amesema dirisha hilo la malipo kitaifa lilifunguliwa rasmi tarehe 28 Oktoba, 2024 mwisho wake ni Novemba 7, 2024 huku akibainisha kuwa katika Hamashauri ya Wilaya ya Mvomero ina walengwa 6130 ambapo kati yao walengwa 3593 wamepokea fedha tasilimu kiasi cha shilingi 108,832,000 na kiasi cha shilingi 76, 466,000 zimelipwa kwa walengwa 2537 kwa njia ya mtandao yaani kwa njia ya benki na mitandao ya simu.
Aidha, ameongeza kuwa Serikali inandelea kuhamasisha walengwa ambao bado wanapokea fedha tasilimu kuunganishwa kwenye mtandao ili waweze kupokea fedha zao kupitia benki au mitandao ya simu kwani kwa njia ya mtandao walengwa wanapakea fedha zao mapema ukilinganisha na wanaopokea fedha tasilimu.
Akielezea faida za malipo ya walengwa kwa njia ya mtandao Afisa Ufuatiiaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Bw. Mweta Kharidi amesema njia hiyo inafaida kwa Serikali na kwa walengwa wenyewe. Kwa upande wa Serikali inasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa mradi ikiwemo kulipa askari, kulipa kamati za usimamizi ngazi ya jamii (CMC).
Nao baadhi ya wanufaika wa mpango huo akiwemo Bi. Fadhila Shomari Mkazi wa Kijiji cha Mbogo ameishukuru Serikali kwa kuanzisha mradi huo ambao umemsaidia kujenga nyumba ya chumba kimoja.
Nae Bw. Abdallah Matuwa amesema kupitia TASAF ameweza kujenga nyumba na amenunua baiskeri hivyo ameishukuru Serikali kuwawezesha kiuchumi.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.