SERIKALI YAAGIZA MIRADI VIPORO IKAMILIKE KABLA YA DISEMBA 30, 2024.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli amewataka Wahe. Madiwani wa Halmashauri hiyo kusimamia miradi ya maendeleo mbayo inatekelezwa katika Kata zao kuanzia miradi ya mwaka 2021 hadi 2024 ili iweze kukamilika kabla ya mwezi Disemba 2024.
Mhe. Nguli ameyasema hayo Agosti 28, mwaka wakati akitoa salamu za Serikali kwenye mkutano wa mwaka wa baraza Madiwani ulio lenga kujadili taarifa za robo ya nne Aprili – Juni uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) kupitia mkutano aliofanya na Wakuu wa Wilaya kwa njia ya mtandao aliagiza miradi ambayo hadi sasa haijakamilika ikasimamiwe ili kuhakikisha kuwa miradi hiyo inakamilika na inatoa huduma kwa wananchi hivyo, amewataka madiwani hao kusimamia miradi hivyo kwa kuwa inatekelezwa katika maeneo yao.
“…niwaombe Waheshimiwa Madiwani mna miradi kwenu, mkaisimamie miradi hiyo…” amesema Mkuu wa Wilaya.
Aidha, Mhe. Nguli amewataka kuwasilisha changamoto ambazo zinasababisha miradi hiyo kutokamilika kwa wakati.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.