Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Mussa Ali Mussa ameonesha kuridhishwa na mradi wa Uboreshaji wa Misitu unaotekelezwa chini ya shirika la PAMS Foundation katika Kata ya Pemba
Wilayani Mvomero, huku akimuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kushughulikia suala la upatikanaji wa hatimiliki za kimila kwa wananchi bila kujali kama ni wanufaika wa mradi huo.
Dkt. Mussa ametoa agizo hilo Julai 17, 2025, alipotembelea Kitongoji cha Disanga kwa lengo la kukagua maendeleo ya mradi huo unaolenga kurudisha uoto wa asili kupitia upandaji wa miti.
Katibu Tawala huyo amebainisha kuwa mradi huo umeonesha manufaa kwa wakazi wa eneo ambalo mradi unatekelezwa kutokana na kuwapatia fursa mbalimbali ikiwemo ajira za muda, elimu ya uzalishaji wenye tija pamoja na elimu ya uhifadhi wa misitu. Aidha, amelipongeza shirika PAMS kwa kuja na wazo la mradi huo.
"...mimi niwashukuru sana hawa wenzetu wa PAMS kwa kuleta huu mradi wa kuhifadhi misitu...niseme wamefanya kazi nzuri...agizo langu mimi hata kwa wale ambao hawapo katika mpango huo wa PAMS na wao ufanye mpango wapewe hati zao za kimila kutokana na maeneo waliyokuwa nayo..." amesema Dkt. Mussa.
Aidha, amewapongeza wananchi kwa kukubali na kuupokea mradi huo ambao una manufaa si tu kwenye mazingira bali na kiuchumi pia huku akiwataka kuendelea kutoa ushirikiano.
Kwa upande wake, Msimamizi wa mradi huo kutoka shirika hilo Bw...amesema kuwa jumla ya mashamba 538 ya wanufaika yenye jumla ya ekari 1560 yamepimwa na kuingizwa kwenye mradi huo, pia amebainisha kuwa kupitia mradi huo wanufaika 347 wamelipwa kiasi cha shilingi milioni 250 ikiwa ni fedha za ushiriki katika mradi pamoja na fidia ya mazao ya kudumu kwa mashamba yaliyo katika eneo la mradi.
Ameongeza kuwa hadi sasa jumla ya miche ya miti 11000 imezalishwa ambapo miche 6000 imetolewa kwa Halmashauri na miche 5000 imetolewa kwa taasisi mbalimbali zilizopo katika Kata ya Pemba.
Wananchi wamenufaika wa mradi huo wamesema PAMS imekuwa mkombozi wa kiuchumi kwa sasa kwani baadhi yao wamepata ajira, imerahisisha upatikanaji wa hati za kimila
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.