Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameupongeza uongozi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe kwa kuendelea kuzalisha wataalam ambao wanaihudumia nchi na maeneo mengine.
Pongezi hizo amezitoa leo Agosti 4, 2024 wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya chuo hicho katika eneo la Maekani.
Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema wapo viongozi wengi ambao ni tunu kwa Taifa wametoka katika chuo hicho akiwemo Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Ombeni Sefue.
Pia ameupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kutumia fedha kutoka vyanzo vya ndani kwa ajili ya kuanzisha ujenzi huo. Aidha, amesema Serikali kupitia Mradi wa HIT inatarajia kutoa fedha zaidi ya bilioni 40 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa chuo hicho cha Mzumbe.
Naye, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Adolf Mkenda (Mb) amemshukuru Rais Samia kwa ujenzi wa miundombinu ya vyuo vikuu karibia mikoa yote hapa nchini huku akisema kuwa Serikali inatambua changamoto za vyuo vikuu ikiwemo uchache wa ofisi, mabweni na madarasa.
Ujenzi huo unahusisha mabweni, ofisi za waadhiri na madarasa.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.