Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea kuonyesha dhamira yake ya kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi kwa kuimarisha mazingira ya kazi ya watendaji wa kata wilayani Mvomero.
Hayo yamebainishwa Januari 20, 2025 na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mwl. Linno Mwageni ameishukuru serikali kwa hatua hiyo muhimu huku akiwataka watendaji waliopokea pikipiki hizo kuhakikisha kuwa zinatumika ipasavyo kwa lengo la kuwahudumia wananchi kwa haraka na kwa tija.
Mwl. Linno ameongeza kuwa hizi ni hatua za kuhakikisha utendaji kazi unakuwa wa ufanisi zaidi, Pikipiki hizo zitawasaidia kufika kwa urahisi katika maeneo ya vijijini, ambako huduma zimekuwa zikikumbwa na changamoto za miundombinu duni.
Kwa upande wao Watendaji wa kata walipokea pikipiki hizo kwa furaha na shukrani, wakibainisha kuwa vitawasaidia kufanikisha majukumu yao, ikiwa ni pamoja na kushughulikia changamoto za kijamii, kusimamia miradi ya maendeleo, na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Pikipiki hizo zimegawanywa kwa watendaji wa Kata za Homboza, Kinda na Kweuma.
MWISHO
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.