Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanayotekeleza miradi yake katika Wilaya ya Mvomero yametakiwa kujielekeza katika kutumia mbinu endelevu za utekelezaji wa miradi ili kuhakikisha matokeo chanya yanayodumu kwa muda mrefu katika jamii.
Wito huo umetolewa Agosti 6, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Maulid Dotto wakati wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ambalo lililenga kutathmini mchango wa Mashirika hayo katika maendeleo ya taifa 2020/2021 - 2024/2025 kwa kuangazia mafanikio, changamoto, Fursa na matarajio.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa kwa kiasi kikubwa mashirika hayo yamekuwa na mchango mkubwa katika kuwaimarisha wananchi kiuchumi kupitia miradi waliyoianzisha katika maeneo mbalimbali Wilayani humo, huku akitumia fursa hiyo kuyapongeza Mashirika hayo.
Aidha, amesema kuwa baadhi ya miradi imekuwa ikitekelezwa kwa muda mfupi hasa miradi ya kuwainua vijana kiuchumi huku miradi mingine kufa baada ya mashirika hayo kukamilisha muda wa utekelezaji kutokana na ukosefu wa mbinu endelevu, hivyo ameyataka Mashirika hayo kujikita katika mbinu za kuendeleza miradi inayoanzishwa.
Hata hivyo Mhe. Maulid amebainisha baadhi ya mbinu ambazo zinaweza kusaidia miradi hiyo kuwa endelevu ikiwemo kushirikiana kwa karibu na jamii husika, serikali za mitaa na wadau wengine ili kuhakikisha miradi inayotekelezwa inaendana na mahitaji halisi ya wananchi na inaungwa mkono na wanufaika wake.
Ameongeza kuwa ni muhimu kwa NGOs kujikita kwenye kujenga uwezo wa jamii kujisimamia, kuwajengea stadi na maarifa, pamoja na kuweka mikakati ya upatikanaji wa rasilimali kwa ajili ya kuendeleza miradi hata baada ya ufadhili kuisha.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Ndg. Paulo Faty amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi ambayo yanaruhusu Mashirika yasiyo ya Kiserikali kutekeleza shughuli zake.
Naye, Mwenyekiti wa Baraza la umoja wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NACONGO) Mkoa wa Morogoro Bw. Otanamusu Masaoe amebainisha kuwa Wilaya ya Mvom
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.