Naibu Waziri Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Joseph Kakunda amefanya ziara ya siku moja kutembelea wilayani Mvomero na kukagua maendeleo ya miradi ambayo Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero imekuwa ikitekeleza chini ya usimamizi wa Serikali tarehe 3 Agosti 2018.
Miradi ambayo imetembelewa ni pamoja na Hospitali ya Wilaya ya Mvomero ambayo ujenzi wa jengo la Utawala umekamilika kwa asilimia 100 pamoja na Ujenzi unaoendelea wa Shule ya Sekondari ya Kumbukumu ya Sokoine ambayo ujenzi wake pia unaendelea.
Awali akisoma taarifa kwa Mheshimiwa Naibu Waziri, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Ndg, Florent Kyombo amesema kwamba ujenzi wa Jengo la Utawala umekamilika na wanasubiri fedha kutoka serikalini ili waweze kuongeza baadhi ya majengo muhimu ili kusogeza huduma ya Afya kwa wananchi wa Mvomero na maeneo ya karibu.
Aidha kwa upande wa Shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Sokoine Mkurugenzi amemuhakikishia Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba wanategemea kukamilisha ujenzi wa shule hiyo mara tu baada ya kupokea fedha kutoka Serikalini na kwamba tayari ujenzi wa jengo la utawala pamoja na baadhi ya nyumba za walimu umekamilika huku wakijitahidi kukamilisha ujenzi wa madarasa, mabweni, bwalo la chakula pamoja na majengo mengine ili waweze kupokea wanafunzi wa kidato cha 5 kwa muda unaotakiwa.
Akikamilisha ziara hiyo Mheshimiwa Naibu Waziri amepongeza juhudi zinazoonyeshwa na uongozi wa Wilaya hiyo kwa usimamizi mzuri wa miradi na ukamilishwaji wa miradi kwa gharama ambazo zinaleta tija. Ameahidi kwamba hivi karibuni Serikali italeta fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Wilaya pamoja na Shule ya kumbukumbu ya Sokoine kwani Serikali iliamua kujengashule hiyo eneo hilo ili kuenzi mchango wa Hayati Edward Sokoine katika kuleta maendeleo kwa Watanzania.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.