Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mwl. Linno Mwageni mapema hii leo Septemba 30, 2024 amefungua rasmi semina kwa ajili ya wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa ngazi ya Kata na Vijiji.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mwl. Linno amewataka wasimamizi hao kuwa waadilifu na kusimamia haki wakati wote wa mchakato wa uchaguzi. Aidha, amewaelekeza kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa kuzingatia kanuni, sheria, na taratibu zilizowekwa ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uwazi, haki, na usawa.
Sambamba na hayo, Msimamizi huyo wa Uchaguzi amewaonya dhidi ya upendeleo wa aina yoyote na kuwasisitizia umuhimu wa kudumisha amani na usalama wakati wa uchaguzi. Pia ameeleza kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa kuwaandaa kikamilifu katika kusimamia uchaguzi kwa ufanisi.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika Novemba 27, 2024 ukiwa na kaulimbiu isemayo "Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki Uchaguzi".
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.