Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Wilaya Ndugu Maneno Chisepo akiambatana na wajumbe wa kamati hiyo,hivi karibuni walitembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa mwaka wa fedha 2017/2018 katika Halmashauri .
Jumla ya miradi ya maendeleo kumi na sita (16) ilitembelewa na kukaguliwa na kamati hiyo ambayo ni; Mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Pemba ambapo upo katika hatua ya lenter, ukarabati na ujenzi wa kituo cha afya Kibati, mradi wa maji wa Hoza /Salawe, Zahanati ya Difinga, mnada wa Mziha, mradi wa Skimu ya umwagiliaji Lukenge, Soko la mazao Madizini, kuweka mashine na ghala kijiji cha Bungoma kata ya Mkindo kupitia mradi wa PHRD, Skimu ya umwagiliaji Msufini, Zahanati Lukunguni Kata ya Kikeo, Shule ya Msingi Kododo Kata ya Luale, Shule ya msingi Kibuko Kata ya Nyandira ujenzi wa matundu ya vyoo, machinjio Changarawe Kata ya Mzumbe, Soko la mazao Tangeni Kata ya Mzumbe, Mradi wa barabara ya Langali - Nyandira urefu wa Km. 5.2,
Hii ni Shule ya Msingi Pemba yenye jumla ya wanafunzi 982, wavulana 486, wasichana 496 na walimu 11, walimu wanaume 9 na walimu wanawake 2.
Hali ya miundombinu katika Shule ya Msingi Pemba haitoshelezi kulingana na mahitaji yaliyopo; matundu ya vyoo na nyumba za walimu hazitoshelezi kulingana na mahitaji ya Shule. Shule inahitaji madarasa 21, yaliyopo kwa sasa ni 4, pungufu ni 17. Wananchi wa Pemba walianzisha ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa kwa kuchangishana hadi kufikia hatua ya boma ili kupunguza msongamano wa wanafunzi katika madarasa machache waliyonayo kwa sasa.
Ujenzi wa maboma haya umegharimu kiasi cha Shilingi milioni sita na laki tano (6,500,000/=) ambapo Mfuko wa jimbo ulichangia Tshs. 2,000,000/=na nguvu za wananchi ni Tshs. 4,500,000/=
Ili kukamilisha ujenzi wa maboma hayo inahitajika jumla ya Tshs. 15,890,000/=. Serikali ya Kijiji cha Pemba imewasilisha maombi ya fedha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo, maombi hayo yakiwa nje ya mpango wa bajeti wa mwaka fedha 2018/2019.
Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya Wilaya Mvomero baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mvomero Ndugu Florent Laurent Kyombo, walikagua ujenzi huo wa vyumba vya madarasa na kuwapongeza wanakijiji na walimu kwa kazi nzuri ya ujenzi wa maboma hayo ya madarasa, pia walimuagiza Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha wanapata fedha katika vyanzo vya ndani ili kumalizia majengo hayo na ifikapo Januari 2019, yaanze kutumika.
Kamati ya Siasa ikifanya ukaguzi wa Boma
Mkurugenzi Mtendaji (wa Pili kutoka kushoto) Akisoma taarifa ya utekelezaji wa Mradi
wa Ujenzi wa Maboma ya vyumba viwili vya Madarasa katika shule ya Msingi Pemba,
iliyopo kata ya Pemba.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.