Mwenge wa Uhuru Umeendelea kukimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero baada ya kupokelewa kutoka Wilaya ya Gairo,ambapo uliweka mawe ya msingi,kufungua miradi,kukagua na kutembelea miradi ya maendeleo.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mwenge wa Uhuru ulikimbizwa mnamo tarehe 23/07/2018 ambapo jumla ya miradi 6 yenye thamani ya Bil 5,056,069,253.81 ilipitiwa na mwenge wa Uhuru.
Katika miradi hiyo 6 iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Mvomero wananchi walichangia kiasi cha shilingi 39,100,000,Halmashauri shilingi 313,958,000.00 na Serikali kuu shilingi 3,403,739,458.81,wadau wa maendeleo 1,999,811,795.00 ambapo thamani ya miradi yote ni Bil 5,056,069,253.81
Akitoa ujumbe wa Mbio za Mwenge Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018 Ndg.Charles Kabeho aliwasisitiza wananchi kuwekeza katika Elimu ili kuinua uchumi wa nchi yetu. Aidha, aliwasisitiza wananchi kuhamasika katika shughuli za kiuchumi ili kujiletea maendeleo na kuachana na shughuli zisizokuwa na tija kama kujihusisha na kilimo cha bangi ambayo ni madawa ya kulevya.
Aidha Ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 ni "Elimu ni Ufunguo wa maisha Wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu",Kiongozi wa mbio za Mwenge Ndg Kabeho ameendelea kusisitiza wazazi kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kuwapeleka watoto shule na kuwekeza katika kuwasomesha watoto .
Mwenge wa Uhuru mara baada ya kumaliza mbio zake Wilayani hapa umekabdidhiwa Wilaya ya Morogoro tarehe 24 Julai, 2018.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.