Waziri wa Nchi –Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jafo amewataka wadau mbalimbali kuendelea kuchangia sekta ya elimu ili kuiunga mkono Serikali katika kuinua ubora wa elimu nchini.
Mheshimiwa waziri ameyasema hayo hivi karibuni wakati alipotembelea wilayani Mvomero na kukabidhiwa madawati 70 yenye thamani ya shilingi milioni 5 na Mamlaka ya Chakula na Dawakwa ajili ya matumizi ya shule za msingi wilayani humo.
Mheshimiwa Jafo ameipongeza mamlaka hiyo kwa kuweza kutoa msaada wa madawati na kuwataka wadau wengine kuiga mfano wa kuchangia vifaa mbalimbali ili kuiunga mkono serikali katika juhudi zake za kuinua sekta ya elimu hapa nchini.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Bi. Agnes Kijo amesema wao kama TFDA wamepokea pongezi hizo za Mheshimiwa waziri na wataendelea kutoa misaada mingine ili kuiunga mkono serikali.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.