Wilaya ya Mvomero imeweka mikakati kabambe kukabiliana na vitendo vya uhalifu vinavyoendelea kuathiri wananchi Wilayani humo hususan wananchi wa Kata ya Mtibwa.
Hayo yamebainishwa Oktoba 15, 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mhe. Judith Nguli wakati akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Mjimpya kilichopo katika Kata hiyo mkutano uliolenga kuhamasisha wananchi kujiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu.
Mhe. Nguli amesema serikali imejipanga kwa kushirikiana na vyombo vya usalama na wananchi ili kuhakikisha amani na usalama vinadumishwa kwa kuwa Kata hiyo ya Mtibwa ina zaidi ya wananchi 38000 ambao wanachangia kwa kiasi kikubwa kwenye mapato ya Halmashauri ya Mvomero kuliko kata nyingine.
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya ameeleza hatua zilizopangwa ikiwa ni pamoja na kuimarisha doria za polisi na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutoa taarifa za uhalifu mapema. Pia, viongozi wa serikali za mitaa watashirikishwa zaidi katika kuhamasisha vijana kujiunga na miradi ya maendeleo badala ya kujihusisha na vitendo vya kihalifu.
Ameongeza kuwa serikali haitavumilia vitendo vya uhalifu na atahakikisha wahalifu wote wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Pia, ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na vyombo vya usalama kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kukamata wahalifu na kupunguza uhalifu katika wilaya hiyo.
MWISHO.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.