Kilele cha sherehe za Nanenane Kanda ya Mashariki kimefanyika leo tarehe 8 Agosti, 2025 katika viwanja vya Mwl. Nyerere yakihitimisha maonesho ya ubunifu na tecknolojia mbalimbali za kilimo, ufugaji na uvuvi.
Katika maonesho hayo Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero imeibuka mshindi wa Tatu kwenye maonesho ya Nane nane Kanda ya Mashariki Mkoa wa Morogoro, mshindi wa kwanza kwa upande wa mfugaji bora ngazi ya Halmashauri na imeshinda mvuvi bora kutoka Mkoa wa Morogoro.
Bodi ya pamba pia imetoa zawadi kwa wakulima bora wa pamba waliofanya vizuri katika kilimo cha pamba kwa kuzalisha kilo nyingi za pamba ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero imepata zawadi katika kipengele cha washindi wa kanda ya Morogoro.
Shiriki uchaguzi kwa maendeleo endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Wami Sokoine, Dakawa, Mvomero
Anwani Ya Posta: P.O BOX 663, MOROGORO
Msaada wa Kiufundi: +255 23 293 4348
Mobile: +255 23 293 4348
Baruapepe: ded@mvomerodc.go.tz
Hakimiliki ©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.Haki zote zimehifadhiwa.